Makamu wa
 Rais Mstaafu Dk Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mwenyekiti wa 
Kamati ya Maulidi ya Mfungo Sita Shilali alipowasili katika viwanja vya 
maisara kuhudhuria Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad SAW,kitaifa 
yamefanyika katika viwanja vya maisara Zanzibar
Rais wa 
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, 
akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maulidi ya Mfungo Sita Sherali 
Champsi alipowasili katika viwanja vya maisara kuhudhuria hafla hiyo ya 
Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (A.S.W) Kitaifa yamefanyika Zanzibar 
katika viwanja vya Maisara. 
Rais wa 
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, 
akisalimiana na Meya wa Zanzibar Khatib Abrahaman, alipowasili katika 
viwanja vya maisara kuhudhuria hafla hiyo ya Maulid ya Kuzaliwa Mtume 
Muhammad (A.S.W) Kitaifa yamefanyika Zanzibar katika viwanja vya 
Maisara. 
Rais wa 
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad na 
Viongozi wa Dini na Serikali wakijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu 
Duniani kuadhimisha Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.A.W yaliofanyika 
katika viwanja vya maisara Zanzibar. wakiwa wamesimami ikisomwa Qasida 
maalum ya ufunguzi wa hafla hiyo.
Kadhi 
Mkuu wa Zanzibar Sh.Khamis Haji Khamis akizungumza wakati wa hafla ya 
Maulidi ya Kuzaliwa Mtume (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya 
maisara Zanzibar.
Ustadh 
Juma Seif Said akisoma Quran Tukufu Surah Luwman wakati wa hafla hiyo ya
 Maulidi ya Kuzaliwa Mtume Muhammad yaliofanyika katika viwanja vya 
maisara Zanzibar.
Kadhi 
Mkuu wa Zanzibar Sh. Khamis Haji Khamis akitia ubani kuashiria kuaza 
hafla ya kusomwa Maulidi ya Mfungo Sita yaliofanyika Kitaifa 
Zanzibar.katika viwanja vya Maisara.kulia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
 wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Naibu Mufti wa Zanzibar 
Sh. Mahmoud Mussa Wadi. 
Wanafunzi wa Madrasatul Nuhu Islamia ya Jangombe Zanzibar wakisoma Qasweeda ya Rabii Swahili. 
Ustadh 
Rashid Hamad Bakari akisoma Barzanji Mlango wa kwanza wakati wa hafla ya
 maulidi ya kuzaliwa Mtume Muhammd (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja 
vya maisara Zanzibar.
Baadhi ya
 Wanafunzi wa Madrasa na Wananchi wa Zanzibar wakihudhuria hafla ya 
Maulid ya Mfungo Sita katika viwanja vya Maisara Zanzibar.
Ustadh Badru Mohammed Haji akisoma maulidi ya Barzanji Mlango wa Pili.
Wanafunzi wa Madressa Ndandarawiya ya Bumbwini Mkoa wa Kaskazini A Unguja. wakisoma Qasweeda.
Ustadh Mzee Juma Mzee akisoma Maulidi ya Barzanji Mlango wa Tatu.
 
 Madressa
 Qadiria Tul Imaan ya Tomondo Zanzibar wakisoma Qassweeda maalum wakati 
wa hafla hiyo ya Maulidi ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.,A.W) katika 
viwanja vya Maisara Zanzibar. 
 Wananchi
 wakiwa katika viwanja maisara wakiitikia Maulidi ya Kuzaliwa Mtume 
Muhammad (S.A.W) yaliofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Maisara 
Zanzibar.
Ustadh Abdul Rahaman Habshi, akisoma Qiyam Talaa pamoja na Madressa Al Nur Islamia ya Mkunazini Unguja Mji Mkongwe. 
                                                                                              Kwa hisani ya ZanziNews
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni