Jeneza
 lenye Mwili wa Marehemu Dotto Mzava likishushwa Kwenye gari maalum mara
 baada ya kuwasili katika kanisa la Wasabato Manzese uzuri kwaajili ya 
sala ya kuombea kabla ya Mwili kusafirishwa kuelekea Wilaya ya Same 
Mkoani Kilimanjaro.
 Mchungaji
  wa kanisa la Adventist wasabato akiendelea na ibada wakati wa ibada ya
  kumuombea marehemu kabla ya kusafirishwa kuelekea Same Kilimanjaro
 Mkurugenzi
 Mtendaji wa Kampuni ya Jamii Media Maxence Mello akitoa historia fupi 
ya Marehemu Dotto Mzava ambae pia alikua mmoja wa watumishi katika 
kampuni hiyo.
Baba
 Mkubwa wa marehemu Dotto Mzava akitoa maneno ya shukrani katika kanisa 
la Kisabato la Manzese Uzuri mara baada ya zoezi la misa kumalizika.
 Heshima za Mwisho zikiendelea kutolewa
 Majonzi na simanzi kwa ndugu wa marehemu
 Mmiliki wa Fullshangwe Blog,John Bukuku akitoa heshima za mwisho 
 Heshima
 za mwisho zikiendelea kutolewa kwa mwili wa marehemu Dotto Mzava kabla 
haujasafirishwa kuelekea Same Kilimanjaro kwaajili ya mazishi
 Mbunge
 wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika akitoa heshima zake za mwisho kwa 
mwili wa marehemu Dotto Mzava kabla ya Kusafirishwa kuelekea Same 
Kilimanjaro kwa mazishi yanayotarjiwa kufanyika kesho
 Mkurugenzi
 mtendaji wa Jamii Media akitoa heshima za mwisho kabla ya mwili wa 
marehemu kusafirishwa Same Mkoani Kilimanjaro mapema leo
 Ibada ikiendelea
 Jeneza
 lenye mwili wa marehemu Dotto Mzava likipandishwa ndani ya gari tayari 
kwa safari ya kuelekea Same Mkoa wa Kilimanjaro leo kwaajili ya mazishi 
yanayotarajiwa kufanyika kesho 
 Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa kanisani 
 Kwaya ya Angaza ikitoa huduma wakati wa ibada ya kumuombea marehemu Dotto Mzava 
Baadhi
 ya ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dotto Mzava wakiwa kanisani 
kwenye ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika kanisa la 
Wasabato la Manzese Uzuri kabla ya Mwili kusafirishwa kwaajili ya kwenda
 kupumzishwa katika nyumba yake ya milele huko Kwao Same Mkoa wa 
Kilimanjaro.Picha na Pamoja Blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni