Mshereheshaji wa Shindano la Mrembo
wa Dunia Steve Harvey ameomba radhi kwa kumtaja mrembo ambaye si
mshindi Miss Ariadna Gutierrez kutoka Colombia kuwa ni mshindi.
Baada ya kosa hilo, Miss Ariadna
Gutierrez alitangazwa kuwa ni mshindi wa pili na kulazimika kukabidhi
taji alilovishwa kwa mrembo kutoka Philippines, Miss Pia Alonzo
Wurtzbach.
#MissUniverse2015 imekuwa ni moja ya
trendi usiku wa jana huku watumiaji wa mitandao ya jamii wasiamini
kilichotokea.
Miss Wurtzbach aliwaambia waandishi
anamtakia hali njema Miss Gutierrez.
Miss Ariadna Gutierrez akivuliwa taji alilokuwa amevishwa
Miss Philippines Pia Alonzo
Wurtzbach akivishwa taji
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni