WALIOWAUWA WATALII WAWILI WA UINGEREZA WAHUKUMIWA HUKUMU YA FEDHA

Wanaume wawili wa Burma wametiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa kuhusika na mauaji ya watalii wawili raia wa Uingereza, mwaka jana.

Jaji amesema watuhumiwa hao Zaw Lin na Wai Phyo waliwauwa Hannah Witheridge, 23, anayetokea Norfolk pamoja na David Miller, 24, anayetokea Jersey.

Miili ya raia hao wa Uingereza ilipatikana kwenye fukwe ya kisiwa cha Koh Tao Septemba mwaka 2014. Mawakili wanaowatetea watuhumiwa hao wamesema watakata rufaa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni