Meza kuu,wa kwanza kulia ni
Meneja wa redio PANGANI FM Maimuna Msangi, wa pili kutoka kulia ni
Mkurugenzi wa shirika la UZIKWASA ambalo limeratibu tamasha hilo VERA
PIEROTH,wa tatu ni Kaimu mgeni Rasmi ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya
Jamii Wilaya ya PANGANI Bi Patricia, na wanne ni Mratibu wa masuala ya
UKIMWI wilaya ya PANGANI.
Mkurugenzi wa shirika la
UZIKWASA, VERA PIEROTH akizungumza jambo wakati wa kuwakaribisha
wananchi wa PANGANI katika tamasha hilo.
Na Mwandishi wetu
Shirika lisilo la kiserikali
Wilayani Pangani la UZIKWASA linalojishughulisha na kuziwezesha kamati
za kudhibiti Ukimwi, VMACK limezawadia kamati bora za kudhibiti ukimwi
Wilayani humo.
Sherehe hizo zimefanyika sanjari na kuwazawadia kijana bora mfano wa kuigwa na mama bora mfano wa kuigwa.
Katika sherehe zilizofanyika kijiji
cha Jaira,K ata ya Madanga wilayani Pangani na kuhudhuriwa na watu
mbalimbali wakiwemo wananchi na viongozi kutoka halmashauri ya Wilaya ya
Pangani mgeni rasmi alikuwa Kaimu Afisa Maendeleo Wilaya ya Pangani,
Bi.Patricia Kinyange.
Akizungumza katika hadhara hiyo Bi.
Kinyange amelipongeza shirika hilo kwa kuzijengea uwezo kamati hizo
ambazo zinafanya kazi kubwa kwa jamii.
“Kwa kweli shirika la UZIKWASA
nawapongeza sana, mnafanya kazi kubwa kwenye jamii ya Pangani na
kwakweli watu wa Pangani wanapaswa kujivunia uwepo wenu. Nimeshangaa
kuona mambo makubwa yanayofanywa na kamati kutokana na elimu
mnayowapatia,mnastahili pongezi kubwa”alisema Bi.Kinyange.
“Mfano mzuri mimi ARUSHA nilipokua
nafanya kazi, kamati zipo lakini kwakweli wamelala,unakuta kamati
inakutana mara mbili kwa mwaka mzima,lakini huku ni zaidi ya mara
kumi,kwakweli nimeshangaa sana,nyinyi ni shirika ambalo linafaa
kuigwa,lakini wanakamati niwaombee mzidishe juhudi msiwaangushe
wanauzikwasa na sisi kama halmashauri tutajitahidi kushirikiana kwa
karibu kabisha na UZIKWASA ili kuendeleza juhudi hizi.”
Katika hatua nyingine mgeni huyo
rasmi amempongeza kijana aliyeibuka mshindi katika shindano la kijana
bora mfano wa kuigwa na kumtaka kuendeleza juhudi zake na kwamba
Halmashauri watamtumia kama darasa kwa ajili ya vijana wengine kujifunza
kutoka kwake.
Kwa upande wao kamati iliyoibuka
mshindi kwa mwaka wa tatu mfululizo kutoka katika kijiji cha Mseko
wamesema umoja na mshikamano ndio nguzo pekee ya ushindi wao,na kwamba
shukrani pekee zinapaswa kwenda kwa UZIKWASA kwa mafunzo na ufuatiliaji
wao kwani ndio vilivyowafanya kutekeleza mipango waliojiwekea kama
wanakamati hadi kuibuka washindi.
‘Naweza kusema kamati yetu imejitoa
sana,wanakamati wanatumia muda wao mwingi wa ziada katika kuhakikisha
tunatekeleza mipango tuliojiwekea,lakini pia msukumo mkubwa ni kutoka
UZIKWASA kwakweli tunawashukuru sana”Alisema Afisa mtendaji mseko.
Kwa upande wake Mratibu wa shughuli
hizo kutoka shirika la UZIKWASA ambaye pia ni Afisa wa mradi wa jinsia
na uongozi wenye mabadiliko, Bi.Salvata Kalanga amesema haikuwa kazi
rahisi kuzipata kamati bora 8,kutokana na ushindani mkubwa uliokuwepo
kwa washiriki 15,lakini wanashukuru kumpata mshindi ambaye wanaamini
anastahili kutokana na kazi waliyoifanya.
Katika sherehe hizo,mshindi wa
kwanza amepata zawadi ya ngao,pamoja na fedha taslimu shilingi laki
sita,mshindi wa pili alipata laki 4 na nusu,na mshindi wa tatu alipata
shilingi laki 4.
Sherehe ya kuzizawadia kamati bora
za kudhibiti UKIMWI hufanyika kila mwaka chini ya shirika la
UZIKWASA,lengo ni kuzipa motisha kamati hizo ili zifanye vizuri zaidi.
Mashindano haya na tamasha hili
husimamiwa na kuwezeshwa na Asasi ya UZIKWASA Pangani kwa lengo na
Kuamsha hamasa, kuchochea, kutafakari na kujifunza na kujenga
uwajibikaji miongoni mwa vijana, akinamama na Kamati za Kudhibiti UKIMWI
jinsia na uongozi za vijiji.
Mashindano haya huanza baada ya
UZIKWASA kuwezesha kamati hizi kwa kuzijengea uwezo na baadae maafisa
wa UZIKWASA kuzitembelea kamati hizo na makundi yaliyotajwa na kupima
utekelezaji wake kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa na kukubaliwa na
wadau hao.
Kamati, vijana, na akina mama
walioanishwa kufanya vizuri hutembelewa na kamati nyingine kuweza
kujifunza kwa pamoja na kujirudhisha kwa utekelezaji wa kamati hizo. Pia
kwa vijana na wakinamama hutembeleana na kupeana taarifa za utekelezaji
na kujifunza kwa pamoja. Kamatai hizo na hao vijana na akinamama
huchujwa na kubaki wachache ambao wanatekeleza vizuri zaidi.
Baada ya zoezi hilo la kutembeleana
walioanishwa huitwa Pangani na kukutanishwa na waamuzi ambao
huwasikiliza na kuchambua washindi.
Mwaka 2015 kamati 12 zilichaguliwa
kuingia kwenye ushindani huo ambazo ni Mseko, Mwembeni, mkwajuni,
mbulizaga, Bweni, mzambarauni, Mtonga, Mikocheni, Langoni,Tungamaa,
Sange na Jaira.
Akina mama bora waliongia sita bora
kati ya 33 ni kutoka Masaika, Kwa kibuyu, Stahabu, Mwembeni, Mtonga na
Langoni. (watatu watazawadiwa)
Vijana bora waliongia sita bora kati ya 33 ni kutoka Msaraza, Kimanga, Mikocheni, Mseko, Boza na Mivumoni.(watatu watazawadiwa).
Mashindano haya yalianzishwa mwaka
2010 ili kuleta msukumo, ushindani na chachu ya utekelezaji wa mipango
ya vijiji ya ukimwi na maendeleo ya kijiji kwa ujumla na kuotesha mbegu
ya uwajibikaji.
Mwaka 2010 Kamati ya Sanga iliibuka
mshindi, mwaka 2011 kamati ya Langoni, iliibuka mshindi, mwaka 2012
kamati ya Langoni iliibuka mshindi tena. Mwaka 2013 kamati ya Mseko
iliibuka mshindi na mwaka 2014 Mseko iliibuka mshindi tena.
Mwaka huu wa 2015 mchuano ulikuwa
mkubwa na kamati zimejituma na kuwajibika katika utekelezaji wa mipango
yao ya maendeleo pamoja na kuyasaidia makundi mbalimbali yenye uhitaji.
Kamati kumi 15 zimetekeleza vizuri.
Kamati 12 zimetekeleza wastani. kamati 6 ikiwepo, Ushongo, Kipumbwi,
Masaika, Kigurusimba, kimang,a na Mivumoni zinahitaji msukumo wa ziada
kwa Kukosa uwajibikaji.
Mashindano haya yameleta msukumo
katika shughuli zote za kiuongozi na maendeleo ya vijiji. Palipo na
uongozi mzuri na utekelezaji mzuri unakuwepo pia.
UZIKWASA itaendelea kuwajengea uwezo
viongozi wangazi zote na wanajamii kuweza kujitathmini, kuzama na
kujichunguza na kuweza kufanyia kazi changamoto za kiuongoza na
kuwezesha maendeleo katika jamii. Suala la kupinga unyanyasaji wa
wanawake na watoto wa kike litapewa kipaumbele.
Kaimu mgeni rasmi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii Bi.Patricia akizungumza na wananchi waliohudhuria katika tamasha hilo.
Burudani ya ngoma ilikua sehemu ya tamasha hilo.
Washehereshaji wa tamasha hilio, Pili Mlindwa na Shabani Kizamba wakiwajibika.
Wanakamati wa kijiji cha Mseko
katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi, na wameibuka
washindi kwa mwaka wa 3 mfululizo.
Mmoja wa wanakamati ya VMACK ya kijiji cha mseko akicheza kwa furaha mbele ya meza kuu baada ya kutangazwa washindi,
Kaimu Mgeni rasmi Bi.Patricia akiwa ameshika ngao ambayo ni zawadi ya washindi wa VMACK kwa mwaka 2015.
Katibu wa kamati hiyo akipokea zawadi, Ngao na Hundi ya shilingi laki sita.
Vijana bora wa mfano wa kuigwa
walioingia katika hatua ya 3 bora, na aliyeibuka mshindi ni kijana
aliyevaa tshirt rangi ya njano.
Wamama walioingia katika tatu
bora mama mfano wa kuigwa, na aliyeibuka mshindi ni mama ambaye
ameshikilia pochi, ambaye anajulikana kwa jina maaarufu kuti kavu.
Hapa akipokea zawadi ya hundi ya shilingi laki 1 kwa kua mama/mwanamke bora mfano wa kuigwa kwa mwaka 2015.
Mwenyekiti wa kijiji cha Jaira
akigawa zawadi ya sare za shule kwa viongozi wa vijiji vyote vya Wilaya
ya PANGANI kwa niaba ya Aliyekua kijana bora mfano wa kuigwa mwaka
2013-2014,ambayo aliahidi kwa watoto yatima alipochaguliwa.
Wamama wakifurahia jambo.
Sehemu/baadhi ya wananchi
waliohudhuria katika tamasha la kuzizawadia kamati bora za kudhibiti
UKIMWI, kijana bora na mama bora wa mfano wa kuigwa kwa mwaka 2015
zilizofanyika katika kijiji cha JAIRA kata ya MADANGA Wilayani PANGANI.
Waandishi wa habari kutoka redio
PANGANI FM, iliyochini ya shirika la UZIKWASA wakifuatilia kwa makini
tamasha hilo (waliovaa tshirt za PANGANI FM).
Wananchi wa Pangani waliofika katika kijiji cha Jaira wakifuatilia kwa ukaribu tamasha hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni