Rais
Dkt. John Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Charles Kitwanga (Mb) Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Ikulu jijini Dar es salaam leo. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi
Ombeni Sefue.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan (kushoto) akimpongeza
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, mara baada ya kuapishwa Ikulu
jijini Dar es Salaam leo.
Waziri
Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa (kushoto) akimpongeza Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es
Salaam leo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akiteta jambo na Katibu
Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (kulia) na Naibu Katibu Mkuu, John
Mngodo mara baada ya kumpongeza Waziri huyo mpya, nje ya Ukumbi wa Mikutano
Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kulia) akimkaribisha
wizarani Waziri mpya wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga mara baada ya
kuapishwa Ikulu, jijini Dar es Salaam leo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto) akimkaribisha
Waziri mpya wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, ndani ya ofisi ya
waziri huyo iliyopo Mtaa wa Ohio, jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akisaini kitabu cha wageni
kilichopo ndani ya ofisi yake, mara baada ya Waziri huyo mpya kuingia ndani ya
ofisi hiyo baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili kushoto)
akimfafanulia Waziri mpya wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (kulia), shughuli
mbalimbali zinazofanywa na wizara hiyo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, John
Mngodo. Tukio hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo jijini
Dar es Salaam, mara baada ya Waziri huyo kuapishwa Ikulu leo.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akijadiliana na watendaji wa wizara
hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya wizara hiyo, mara baada ya Waziri huyo
kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Wanne kushoto ni Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo,
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), John Minja, Naibu Mkuu wa Jeshi
la Polisi (D/IGP), Abdurahman Kaniki na Kamishina wa Fedha na Utawala wa Idara
ya Uhamiaji, Piniel Mgonja (hayupo pichani).
Picha zote na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano-MOHA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni