Waziri
 wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu 
akizungumza na mmoja wa wahudumu wa afya (jina lake halikuweza 
kupatikana kiurahisi) wa dirisha la dawa katika Hospitali ya rufaa ya 
Bombo mkoani Tanga alipofanya ziara ya kushtukiza mchana wa leo Disemba 
20, 2015.
Waziri
 wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu 
akizungumza na mmoja wa wakina mama anayemhudumia mwanae katika wodi ya 
watoto Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga alipofanya ziara ya 
kushtukiza leo mchana Disemba 20, 2015.
Waziri
 wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu 
akimsikiliza mmoja wa akina mama aliyelazwa kwenye wodi ya wazazi wakati
 wa ziara ya kushtikiza aliyoifanya mchana wa leo Desemba 20, 2015 
katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga.
Kaimu
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO), Dkt. Clement Marceli akimwelezea 
changamoto wanazokabiliana nazo katika Hospitali ya rufaa ya Bombo 
mkoani Tanga Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto,
 Mh. Ummy Mwalimu (hayupo pichani).
Daktari
 aliyekuwa kwenye mafunzo, Dkt. Zuberi (Medical Intern) akitoa maelezo 
ya namna wanavyohudumia wananchi wanaofika hospitalini hapo Waziri wa 
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu 
(kulia) aliyefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya rufaa ya 
Bombo, mkoani Tanga mchana wa leo Desemba 20, 2015 ambapo Waziri huyo 
alikutana na changamoto utoro wa madktari wa zamu kutokuwepo kwenye 
kituo chao cha kazi katika Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga.
Mratibu
 wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo, mkoani Tanga kutoka Idara ya Tiba, 
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. 
Ibrahimu Maduhu (mwenye tai) akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya, 
Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu namna 
wanavyokabiliana na changamoto ya kuzuia vifo vya mama na mtoto katika 
hospitali hiyo wakati wa ziara ya kushtukiza iliyofanywa na Mh. Ummy 
Mwalimu katika wodi ya wazazi leo mchana Disemba 20, 2015.
Baadhi
 ya madaktari waliokuwa mafunzoni wakizungumza na Waziri wa Afya, 
Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu  aliyefanya
 ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo, mkoani Tanga 
mchana wa leo Disemba 20, 2015.
Waziri
 wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu 
akipitia orodha ya mahudhurio ya zamu za Madaktari na Wauguzi ambao 
wengi hawakuwepo kazini wakati wa ziara yake ya kushtukiza katika 
Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga aliyoifanya leo mchana Disemba
 20, 2015.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni