Fundi wa ndege wa shirika la ndege
la Air India amekufa baada ya kuvutwa ndani ya injini ya ndege katika
uwanja wa Mumbai.
Ajali hiyo imetokea wakati ndege
aina ya AI 619 kutoka Mumbai kwenda Hyderabad ikirudi nyuma kujiandaa
kuondoka, kwa mujibu wa shirika la Air India.
Mwenyekiti wa shirika la Air India
Ashwani Lohani ameeieleza ajali hiyo kuwa ni ya bahati mbaya, lakini
haijajulikana wazi nini kilitokea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni