Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Ally Mwalimu
akiingia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) leo asubuhi kwa
ajili ya kukagua utengenezaji wa mashine ya MRI na CT- Scan.
Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Mwalimu akiwa
na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Mseru leo asubuhi
katika hospitali hiyo.
Mtaalamu
wa Mionzi kwenye chumba cha mashine ya MRI, Job Joshua (kushoto) na
Profesa Mseru (wa pili kulia) wakimpatia maelezo Waziri Ummy Mwalimu
(katikati) wakati alipotembelea leo hospitali hiyo kukagua utengenezaji
wa mashine hiyo.
Mkuu
wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare akitoa maelezo kwa Mheshimiwa
Waziri kuhusu maendeleo ya utengenezaji wa mashine ya MRI leo asubuhi.
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu (katikati) akiwa na Profesa Mseru kuelekea kwenye chumba cha X-ray cha digitali.
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu akizungumza leo asubuhi na wagonjwa wanaosubiri vipimo katika hospitali hiyo.
Mheshimiwa
Waziri Ummy Mwalimu akiwa katika chumba cha CT-SCAN, huku Mkuu wa Idara
ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare akimpatia maelezo jinsi mashine hiyo
inavyofanya kazi wakati ikiwa nzima.
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu akifafanua jambo baada ya kupewa maelezo jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Lawrence Mseru (kulia), Mheshimiwa Waziri,
Ummy Mwalimu (katikati) wakimsikiliza mgonjwa aliyefika katika hospitali
hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu leo asubuhi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni