Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu wakati alipokuwa
anawasili Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam kwa ziara ya
kikazi. Waziri Kitwanga alifanya mazungumzo na Viongozi Wakuu wa jeshi
hilo na kukubaliana kuweka mikakati zaidi ya kukabiliana na uhalifu
nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akitoa taarifa mbalimbali
za shughuli zinazofanywa na jeshi hilo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Charles Kitwanga (katikati), wakati Waziri huyo alipofanya ziara
Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuzungumza
na Viongozi Wakuu wa jeshi hilo, ambapo walikubaliana kuweka mikakati
zaidi ya kukabiliana na uhalifu nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mazungumzo na Viongozi
Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini. Waziri Kitwanga aliwaambia waandishi wa
habari kuwa, wamekubaliana na Viongozi Wakuu wa jeshi hilo kuweka
mikakati zaidi ya kukabiliana na uhalifu nchini. Wapili kushoto meza kuu
ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Wapili kulia meza
kuu ni Naibu IGP, Abdulharam Kaniki. Kulia ni Kamishna wa Oparesheni na
Mafunzo wa Jeshi hilo, Paul Chagonja. Kushoto meza kuu ni Kamishna wa
Polisi Jamii nchini, Mussa Ali Mussa. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa
Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Suleiman
Kova.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati waliokaa), Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (watatu kulia waliokaa)
wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wakuu wa Jeshi la Polisi
nchini mara baada ya kikao chao kilichofanya katika Ukumbi wa Mikutano
wa Makao Makuu ya Jeshi hilo kumalizika. Waziri Kitwanga alifanya
mazungumzo na Viongozi hao na kukubaliana kuweka mikakati ya kupambana
na uhalifu.
Msafara
wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ukiwasili katika
lango Kuu la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam kwa
ajili ya kufanya mazungumzo na Viongozi Wakuu wa Jeshi hilo. Picha zote
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni