Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akimsalimia
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile wakati alipowasili
Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya
ziara ya kikazi. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak
Abdulwakil, na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo. Katika ziara
hiyo, Waziri Kitwanga aliitaka Idara hiyo ya Uhamiaji kuanz rasmi kwa
operesheni ya kuwakamata Wahamiaji Haramu nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (aliyevaa tai) akiwasalimia
wananchi wanaosubiri kupata huduma ya Hati za Kusafiria katika Ofisi za
Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Waziri
Kitwanga alifanya ziara ya kikazi katika ofisi hizo kwa lengo la
kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na Uhamiaji. Katika hotuba yake,
licha ya maelekezo mengine aliyoyatoa kwa viongozi wakuu, pia aliitaka
Idara hiyo ya Uhamiaji kuanza rasmi kwa operesheni ya kuwakamata
Wahamiaji Haramu nchini.
Afisa
Uhamiaji anayeshughulika na uchapaji wa Hati za Kusafiria, Amir Hassan
(kushoto), akitoa maelezo ya jinsi wanavyozichapisha Hati za Kusafiria,
kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati)
ambaye alifanya ziara ya kikazi katika ofisi za Makao Makuu ya Uhamiaji,
Kurasini, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji, Sylvester Ambokile.
Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile (kushoto) akiwa na Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, wakati Waziri huyo alipokuwa
anafanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar
es Salaam kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na
Uhamiaji.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwaeleza jambo
Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati alipofanya ziara ya kikazi
Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam leo. Wapili
kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak
Abduwakil, na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, John Mngodo,
na wapili kulia (waliokaa) ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester
Ambokile na kulia ni Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha), Piniel
Mgonja.
Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile akimfafanulia jambo Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) wakati Waziri huyo
alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar
es Salaam leo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wasita kulia), Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (watano kushoto), Naibu Katibu Mkuu,
John Mngodo (wanne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi
Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati Waziri huyo alipotembelea Makao Makuu
ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam. Wasita kushoto ni
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile. Picha zote na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni