Waziri
 wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kanda na 
Kimataifa,Balozi Augustine Mahiga(kulia)akiwasili kwenye kituo cha 
mikutano cha kimataifa cha Arusha International Conference Center(AICC) 
ambacho ni sehemu ya Wizara hiyo,kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa 
AICC,Elishilia Kaaya. 
Waziri
 wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kanda na 
Kimataifa,Balozi Augustine Mahiga akisaini kitabu cha wageni. 
Mkurugenzi
 Mtendaji wa Arusha International Conference Center(AICC)Elishilia 
Kaaya(kulia) akifafanua jambo mbele Waziri Mahiga(kushoto)katikati ni 
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Wilson Kambaku.
Mkurugenzi
 Mtendaji wa Arusha International Conference Center(AICC)Elishilia Kaaya
 akifafanua jambo mbele Waziri Mahiga(wa pili kulia)wengine ni Mkuu wa 
Wilaya ya Arumeru,Wilson Kambaku(kulia)Mwenyekiti wa Bodi ya AICC,Balozi
 Christopher Lihundi(aliyevaa tai) na Mkuu wa mawasiliano 
serikalini,Mindi Kasiga. 
Mwenyekiti
 wa Bodi ya AICC,Balozi Christopher Lihundi akizungumza jambo mbele 
Waziri Augustine Mahiga aliyefika katika kituo hicho tangu ateuliwe 
kushika wadhifa huo. 
Baadhi ya watumishi wa AICC.
Waziri
 wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kanda na 
Kimataifa,Balozi Augustine Mahiga akizungumza na wajumbe wa Bodi ya AICC
 na watumishi wa kituo hicho ,kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya 
AICC,Balozi Christopher Lihundi na kulia ni Mkuu wa wilaya ya 
Arumeru,Wilson Kambaku.
Mkuu wa mawasiliano serikalini, Mindi Kasiga akiongoza kipindi cha maswali kwa waandishi wa habari. 
Waziri
 wa Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki,Kanda na Kimataifa 
,Balozi Augstine Mahiga amesema eneo la Laki Laki lililopo wilaya ya 
Arumeru mkoani Arusha lililotengwa kwaajili ya ujenzi wa taasisi za 
kimataifa utaifanya Tanzania kung'ara duniani.
 
Balozi Mahiga alisema hayo Desemba 19 baada ya kufanya ziara kwenye eneo hilo na Kituo cha mikutano cha kimataifa cha AICC .
 
Eneo
 hilo litajengwa Mahakama ya Kimataifa ya Kimbari(MICT)Mahakama ya 
Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR) na taasisi zingine na kusema 
ameridhishwa na hatua iliyofikiwa.
Akiwa kwenye kituo cha AICC alipokea taarifa za mradi wa ujenzi wa kituo cha mikutano cha kimataifa cha Kilimanjaro International Convention Center kitachovuta dunia Tanzania.
Pia Waziri alizungumzia hali ya kisiasa nchini Burundi kuwa inaigusa Tanzania na kuwa atawasiliana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Dk Richard Sezibera kuandaa kuandaa mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje.
                                            
                                      Imeandaliwa na www.manyaraleotz.blogspot.com

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni