WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII PROF. JUMANNE MAGHEMBE AWASILI MAKAO MAKUU YA WIZARA HIYO MARA BAADA YA KUAPISHWA IKULU LEO


Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (mbele kulia) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Selestine Gesimba wakati wa mapokezi yake leo tarehe 28 Desemba 2015 katika ofisi yake mpya Mpingo House mara baada ya kuapishwa Ikulu mapema asubuhi ya leo. Nyuma yake kulia ni naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Eng. Ramo Makani na anaeongoza utambulisho katikati yao ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akisaini kitabu cha wageni mara tu baada ya kuingia katika ofisi yake mpya iliyopo Mpingo House mapema leo tarehe 28 Desemba 2015 baada ya kuapishwa Ikulu na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Wanaoshuhudia kulia ni Naibu Wazari wa Wizara hiyo Mhe. Eng. Ramo Makani na Katibu Mkuu Dkt. Adelhelm Meru (kushoto).
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru (kushoto) na Naibu Waziri Mhe. Eng. Ramo Makani (kulia) mara baada ya kusaini kitabu cha wageni ofisini kwake mapema leo tarehe 28 Desemba 2015.
Picha ya pamoja kati ya Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia) na Naibu Waziri wake Mhe. Eng. Ramo Makani (wa pili kushoto), Katibu Mkuu wa Wziara hiyo Dkt. Adelhelm Meru (wa kwanza kulia) na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Selestine Gesimba(kushoto). 
Sehemu ya wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa tayari kwa mapokezi ya Waziri wao mpya Mhe. Prof. Jumanne Maghembe aliyeapishwa Ikulu leo na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania Mhe. John Pombe Magufuli.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni