WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) WAHAMASISHA UTALII WA NDANI KWA VITENDO

 Mnyama Ngiri akiwa amejipumzisha kwenye tope kama alivyokutwa na kamera yetu.

Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) wamefanya
ziara ya siku mbili ya kitalii katika hifadhi ya taifa ya Saadani pamoja na sehemu ya kihistoria ya Kaole iliyopo Bagamoyo ikiwa ni sehemu
ya kujifunza pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani.

Wanafunzi hao kutoka katika “Collage” tofauti tofauti ikiwemo utalii , uchumi na biashara waliofanya ziara hiyo ikiwa chini ya mwamvuli wa University of
Dar es Salaam Tourism Association (DUTA) ,walipata fursa ya kujifunza na
kushuhudia wanyama pori pamoja na sehemu ya kihistoria ya Kaole na
kuhamasisha jamii hasa ya wasomi kuwa mfano wa kuigwa kwa kuzuru hifadhi
pamoja na makumbusho ili kuhimiza utalii wa ndani. 
Hii ni tabia ya kipekee ya ngiri ambapo hula nyasi akiwa amepiga mfano wa magoti kwa kukunja miguu ya mbeleWaterbucks kama wanavyojulikana wakiwa miongoni mwa wanyama walioonekana wakati wa ziara hiyo Akizungumzia ziara hiyo aliyekuwa kiongozi wa msafara huo ambaye ni mwanafunzi wa kozi ya utalii ,Gabriel Lyimo alisema huu ni muendelezo wa ziara ambazo wamekuwa wakizifanya kama sehemu ya kujifunza pamoja na kuhamasisha watanzania na hasa wanafunzi pamoja na wasomi kujenga utamaduni wa kukuza pato la taifa kwa kufanya utalii wa ndani na sio kuona kama ni jukumu la wageni. 
                                                                                                     Picha ya pamoja

Sambamba na hilo wanafunzi hao walipata fursa ya kuweka kambi pembezoni mwa mwambao wa bahari ya hindi na kutumia fursa hiyo kupata upepo mwanana , kupumzika na kuogelea.  Saadani National Park ni Hifadhi ya Taifa ya 13 ya Tanzania yenye eneo la 1,062 km za mraba ambapo watalii
wanaweza kuona wanyama pamoja mwambao Bahari ya Hindi.Mbuga hii ilikuwa rasmi katika gazeti la serikali mwaka 2005, Saadani National Park ni hifadhi pekee nchini Tanzania ambayo imepakana na bahari ya Hindi.
 Mtembezi na muelekezi katika hifadhi ya Saadani Bw.Mollel akifafanua jambo wakati wa ziara ndani ya hifadhi  
Baadhi ya wanafunzi wakisikiliza historia kuhusu mji huu wa Saadani huku toka kwa mwenyeji na mkongwe wa eneo hilo mzee Mlelwa (mwenye shati la kijani) wakati wa jioni  
Mambo ya Msosi: baadhi ya wanafunzi wakiwa katika harakati za kuchoma kitoweo kwa ajili ya mlo wa usiku                                                                                                       Hakika anapendeza!! wanafunzi hao wakiwa karibu na eneo ambalo maji kutoka mto wami yanakutana na maji ya bahari ya hindi Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakichagua shanga na vito vya asili walipozuru Kaole Mamba Ranch iliyopo Bagamoyo 
 Moja kati ya mamba wanaopatikana katika eneo la Kaole Mamba Ranch

 
Kwa umakini na huku wakipewa fursa ya kuuliza maswali , wakisikilza historia ya eneo la Kaole na mfululizo wa matukio ya kihistoria kutoka kwa mtaalamu wa historia Bw.Ramadhani  Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa mbele ya msikiti wa kwanza uliojengwa katika pwani ya Afrika ya mashariki Kulingana na historia ya eneo hili ,inasemekana kuwa mbuyu huu umeishi zaidi ya miaka mia tano na wengi wamekuwa wakiamini kuuzunguka mbuyu huu (kutoka upande wa kushoto kwenda kulia) kunaweza kumuongezea mtu miaka ya kuishi. na manyaraleo blog

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni