Kapteni wa zamani wa Cameroon,
Samuel Eto'o ameteuliwa kuwa kocha mchezaji wa muda wa timu ya
Uturuki ya Antalyaspor.
Mshambuliaji huyo alijiunga na klabu
hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu inayoishia Juni mwakani, amepewa
michezo mitatu ya majaribio ili kuuridhisha uongozi.
Eto'o amechukua wadhifa huo kutoka
kwa Yusuf Simsek, ambaye mkataba wake ulikatizwa kwa makubaliano na
uongozi wa timu hiyo Desemba 7.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni