Rafiki mmoja wa wandandoa waliofanya
mashambulizi San Bernardino amefunguliwa mashtaka ya kuhusika na
mauaji ya kutumia risasi ya watu 14.
Mtu huyo Enrique Marquez, miaka 24
anakuwa mtu wa kwanza kufunguliwa mashtaka kwa kuhusika na
mashambulizi hayo mabaya ya kigaidi tangu tukio la Septemba 11.
Bw. Marquez amefunguliwa mashtaka
kupanga mashambulizi ya kutumia bunduki na Syed Farook kwenye chuo
kimoja mwaka 2011 na 2012.
Pia anashtakiwa kwa kununua kinyume
na sheria bunduki mbili aina ya rifles zilizotumiwa kwa mauaji na
Farook na Tashfeen Malik.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni