Katibu Mkuu wa TOC Filbert Bayi
akizungumza na wana Michezo mbalimbali waliohudhuria katika Mkutano
Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika Ukumbi wa kituo cha Utengamano Welezo
Mjini Zanzibar.
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka
waliohudhuria katika Mkutano huo wakisikiliza maelezo kwa Mgeni Rasmi
Katibu Mkuu msaidizi Jamali Nassor Adi hayupo pichani
Mgeni Rasmi Jamal Nassor Adi
akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa kamisheni ya
Wachezaji Tanzania (KAWATA) katika Ukumbi wa Kituo cha Utengamano Welezo
Mjini Zanzibar.
Wajumbe wakiwa katika picha ya Pamoja.
PICHA NA ABDALLA OMAR –HABARI MAELEZO.
…………………………………………………………………………………………………………
Na Rahma Khamis /Miza Othman -Maelezo Zanzibar.
Kamati ya Olimpiki Tanzania
(TOC) wamewataka Viongozi wa Mashirika ya Vyama vya Michezo
Tanzania kusaidiana na wanamichezo mbalimbali ili kufikia hadhi ya
kimataifa .
Hayo yameelezwa na na Katibu
mtendaji wa TOC Jamal Nassor Adi huko Kituo cha Utengamano Welezo
Zanzibar wakati alipokua akifungua Mkutano mkuu wa mwaka wa Kamisheni
ya Wachezaji Tanzania .
Amesema lengo kuu la mkutano huo ni kuhamasisha na kuamsha ari kwa Wachezaji ili kuweza kurejesha hadhi ya Michezo Tanzania.
Katibu Jamal amefahamisha kuwa
wachezaji ndio wahusika wakuu wa michezo hivyo ni lazima kushirikishwa
na kupatiwa elimu ili kuweza kufahamu wajibu wao katika michezo na
kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima.
Akizungumzia suala la dawa za
kuongeza nguvu kwa wanamichezo, Katibu Jamal amesema ni vyema
wachezaji kuzifahamu na kujiepusha nazo kwani kitendo hicho kinaweza
kupelekea nchi kupigwa marufuku kushiriki michezo ya Kimataifa.
Nae Katibu wa Kamati ya Olimpiki
ya Tanzania Filbert Bayi amesema kuwa michezo ni chanzo cha kujipatia
ajira kwa vijana hivyo ni vyema michezo iendelezwe ili kuleta
maendeleo kwa wachezaji wenyewe na Taifa kwa ujumla.
Aidha amesema katika kuimarisha
michezo Nchini suala la kuteuliwa wawakilishi wenye uwezo ni
jambo muhimu na amewashauri washiriki wa mkutano huo kusaidia ili
kupunguza malalamiko.
Mwenyekiti wa Kamsheni ya
Wachezaji Tanzania (KAWATA) Ramadhani Zimbwe ameahidi kupambana na
rushwa kwa viongozi na watendaji wa michezo nchini kwani vitendo hivyo
vinarudisha nyuma ufanisi wa michezo.
Amesema rushwa ni adui wa haki na
mara nyingi hupelekea mtu mwenye uwezo wa kifedha kupata haki
asiyostahiki na kumuacha mwenye haki hiyo kuikosa kutokana na kukosa
fedha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni