FREDRICK MWAKALEBELA AKIWA NA ELISHA MWAMPASHE KATIBU WA CCM WILAYA YA IRINGA MJINI WAKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI.
BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WA MKOANI IRINGA WALIPOKUWA
WANAWASIKILIZA FREDRICK MWAKALEBELA NA ELISHA MWAMPASHE KATIBU WA CCM
WILAYA YA IRINGA MJINI.
Chama
cha mapinduzi wilaya ya iringa mjini kimekanusha kufutwa kwa kesi yao
dhidi ya mkurungenzi wa manispaa hii pamoja na mbunge wa jimbo la iringa
mjini mchungaji PETTER MSINGWA.
Akizungumza na waandishi wa
habari katibu wa ccm wilaya ya iringa mjini ELISHA MWAMPASHE amesema
kuwa taarifa zilizosambaa sehemu mbalimbali sio za kweli.
“Nimekuwa nikipigiwa simu nyingi toka jana nikipewa taarifa kuwa kesi
yetu imetupiliwa mbali na imeenea sana kwenye mitandao ya kijamii na
maeneo mbalimbali ukweli ni kwamba kesi ya uchaguzi namba tano ya 2015
haijafutwa”alisema Elisha mwampashe.
Mwampashe ameongeza kuwa
kesi hiyo bado haijapangiwa siku ya kusikilizwa wala kupangiwa jaji wa
kuendesha kesi hiyo hivyo anashangaa kuaona taarifa zinazendelea kuenena
mitaani.
“Ifahamike kuwa mahakamani kuna
shauri la msingi ambalo lilikuwa na kupinga matokeo na kuna shauri
dogo namba 28 la mwaka 2015 ndio lilikuwa likizungumziwa jana kwa lengo
la kuomba kupunguziwa dhamana kutokana na sheria kuruhusu kufanya
hivyo” alisema Elisha mwampashe.
Mwampashe amemalizia kwa
kuwataka wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi kuendelea kuwa na
subra kwa kuwa haki yao ya msingi itapatikana mahakani na kuwasii
wananchi wanaopotosha taarifa hizi.
kwa upande wake fredrick
mwakalebela aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la iringa mjini amesema kuwa
shauri lilofutwa ni la kuomba kupunguziwa pesa ya dhamana.
“Nilikuwa kimya kutokana na kufatilia swala hili kimya kimya kwa lengo
la kupata haki yangu ya msingi ambayo nimenyang’anywa na mkurugezi wa
manispaa ya iringa pamoja na mchungaji petter msingwa” alisema Fredrick
mwakalebela
Mwakalebela amemalizia kwa kusema kuwa kesi hiyo
inaendeshwa naye pamoja na chama cha mapinduzi kwa kuwa chama ndio
kilichompa nafasi ya kugombea ndio maana kila kitu anachokifanya chma
lazima kijue juu ya kesi hivyo.
ilitolewa taarifa Kuhusu
kutupiliwa mbali kwa shauri ya dhamana ya kesi ya ubunge Iringa Mjini
Msajiri wa Mahakama kuu Iringa Bi Ruth Masamu amesema kesi ya aliyekuwa
mgombea ubunge Jimbo La Iringa Mjini Fredrick Mwakalebela alitoa ombi la
kuomba kupunguziwa dhamana kutoka milioni kumi na kushuka angalau kwa
kiasi kidogo.
Hii ni kutokana na vifungu vya sheria kuruhusu
kuomba ombi hilo na mahakama kulikataa na kumtaka aongeze mtuhumiwa
ambaye ni mwanasheria wa serikali kwenye kesi yake kwa gharama hiyohiyo.
Hivyo uvumi uliotolewa jana kwamba kesi imefutwa si kweli kwa sababu mpaka sasa kesi bado haijapangwa wala kuanza kusikilizwa
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni