Kiongozi wa Upinzani nchini Kenya
Raila Odinga amepongeza uamuzi wa kujiuzulu kwa Waziri wa Wizara ya
Ugatuaji Bi. Anne Waiguru kufuatia wizara yake kukumbwa na kashfa za
ufisadi.
Hata hivyo Raila amemtaka Rais Uhuru
Kenyatta kuwafukuza kazi mawaziri wengine ambao wizara zao
zimekabiliwa na tuhuma za rushwa.
Aidha, Raila amesema
amechanganyikiwa, labda Waiguru na rais Uhuru Kenyatta wampatie
maelezo kutokana na kauli ya waziri huyo kudai afya yake sio nzuri na
atamuomba rais ampagie kazi rahisi, ambapo amesema angependa kujua
kazi hiyo rahisi ni ipi hata kama ni ya jikoni.
Anne Waiguru Waziri aliyejiuzulu wadhifa katika Wizara ya Ugatuaji
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni