Wanajeshi wa Kenya na maafisa polisi
wamepelekwa katika mpaka wa Kenya na Ethiopia eneo la Sololo, katika
Kaunti ya Marsabit baada ya kuuwawa maafisa polisi watatu wa Kenya na
wanajeshi wa Ethiopia siku ya Ijumaa.
Wanajeshi wa Ethiopia waliingia
katika mipaka ya Kenya na kuwauwa kwa kuwapiga risasi maafisa polisi
watatu wa Kenya, kuharibu gari la polisi na kisha kuchukua silaha nne
huko Anona, Kaunti ya Marsabit.
Kamishna wa kaunti ya Marsabit
Moffat Kangi amesema wanajeshi pamoja na polisi wapo tayari wakilinda
usalama katika maeneo ya Ramole na Anona katika mpaka wa Kenya na
Ethiopia, ambapo tayari miili ya maafisa wa polisi waliouwawa
imesafirishwa kwa ndege Nairobi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni