Watu 23 wamekamatwa na makumi ya
silaha kukutwa katika misako kadhaa dhidi ya wapiganaji wa kundi la
Dola ya Kiislama nchini Ufaransa.
Msako huo unafuatia mashambulizi ya
mfululizo kwenye baa, hoteli, ukumbi wa tamasha pamoja na uwanja wa
mpira Jijini Paris siku ya Ijumaa na kuuwa watu 129.
Operesheni hiyo ya msako wa jeshi la
polisi pia inafanyika Jijini Brussels Ubelgiji na kunataarifa kuwa
mtuhumiwa mmoja amekamatwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni