Timu ya Liverpool imeichakaza
Manchester City na kufuta matumaini yake ya kurejea kuongoza Ligi Kuu
ya Uingereza, baada ya kupata ushindi wa mabao 4-1 katika dimba la
Etihad hali inayoashiria kuimarika ikiwa chini ya Jurgen Klopp.
Kikosi hicho cha Klopp kiliwapeleka
puta wenyeji Manchester City ambapo katika kipindi cha kwanza tu
tayari walifunga mabao 3-0, yaliyofungwa na Eliaquim Mangala
aliyejifunga, na kufuatiwa na bao murwa la Philippe Coutinho pamoja
na bao la Roberto Firmino.
Sergio Aguero aliipa matumaini
Manchester City baada ya kufunga goli moja, hata hivyo beki ya timu
hiyo ilionekana kuwa kichochoro baada ya kuumian kapteni wao Vincent
Kompany, na Martin Skrtel alifunga kitabu kwa
kupachika bao la nne.
Mshambuliaji Roberto Firmino akipachika bao
Nayo Chelsea iliambulia ushindi wa
bao 1-0 dhidi ya Norwich, kupitia kwa mchezaji wake Diego Costa.
Matokeo mengine ya ligi hiyo jana ni Watford 1 - 2 Man Utd, Everton
4 - 0 Aston Villa, Newcastle 0 - 3 Leicester, Southampton 0 - 1
Stoke, Swansea 2 - 2 Bournemouthna West Brom 2 - 1 Arsenal.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni