Vijana
wa YAM ( Youth Action Movement) ambao ni waandaaji wa tamasha hili
linalofanyika kila mwezi wakionesha igizo lao lililobeba ujumbe unaosema
ni jukumu la wazazi kuwaelimisha vijana juu ya afya ya uzazi na ujinsia
ili kuwakinga na maambukizi ya VVU mimba katika umri mdogo na ngono
katika umri mdogo.
Mwenyekiti
wa UMATI dar es salaam Mr.Harith Shomvi ambae alikuwa mgeni rasmi
katika tamasha hilo akihutubia wananchi na kuwasisitiza wapate huduma
za uzazi wa mpango na upimaji ambazo zilikuwa zikitolewa bure katika
tamasha hilo. Tamasha hilo lilikuwa na kauli mbiu isemayo "JE kutoa
elimu juu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana ni jukumu la nani?
Baadhi ya
wananchi wakijiandikisha ili waweze kupata huduma ya upimaji VVU na
uzazi wa mpango zilizokuwa zikitolewa bure na UMATI katika tamasha hilo
la jamvi la vijana.
Mtoa huduma wan UMATI Bibi. Neema Orgeness akimpima mteja VVU.
Mtoa
huduma wa UMATI Monika Nkwera akimpatia mama huduma ya uzazi wa mpango
wakati wa Tamasha la Vijana lililofanyika jijini Dar es Salaam mapema
wikiendi hii. Tamasha hilo lilikuwa na kauli mbiu isemayo "JE kutoa
elimu juu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana ni jukumu la nani?
Kikundi
cha nyota kutoka Temeke wakionesha igizo linaloelezea umuhimu wa wazazi
kuwapa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia watoto wao ili kuwaepusha na
ngono katika umri mdogo,mimba katika umri mdogo,VVU/UKIMWI,na pia athari
zingine zitokanazo na ukosefu wa elimu na habari sahihi kuhusu afya ya
uzazi na ujinsia.
Picha na Maelezo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni