Kamanda
wa Kikosi cha Usalama Barabarani,DCP Mohamed Mpinga, akisalimiana na
Mabalozi wa Usalama Barabarani, muda mfupi kabla ya kuzindua Operesheni
ijulikanayo kwa jina la “Paza Sauti” yenye lengo la kuwaelimisha abiria
ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa
sheria za barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam
leo.
Kamanda
wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga, akitoa
maelekezo ndani ya moja ya basi linalofanya safari zake mkoani wakati
wa kuzindua wa Operesheni Paza Sauti yenye lengo la kuwaelimisha
abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona viashiria vya uvunjifu
wa sheria za barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es
Salaam leo.
Wadau
wanaotumia usafiri wa barabara, wakiwemo madereva na abiria
wakimsikiliza Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,
Mohammed Mpinga(hayupo pichani) alipozindua Operesheni Paza Sauti,
yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa wanapoona
kuna viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani,Operesheni hii
ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Tuzo na Matukio wa Mabalozi wa Usalama Barabarani,Jackson
Kalikumtima(kulia), akitoa elimu kuhusiana na Operesheni ya Paza Sauti
kwa mmoja wa wadau wanaotumia usafiri wa barabara, Operesheni hii
ilizinduliwa Stendi ya Mabasi yaendayo mikoani ya Ubungo, jijini Dar es
Salaam leo.(Picha zote na Abubakari Akida,Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni