Msichana mmoja amepigwa mawe hadi
kufa nchini Afghanistan baada ya kutuhumiwa kufanya zinaa.
Video iliyopigwa kuonyesha namna
msichana huyo alivyokuwa akitekelezewa hukumu hiyo imewekwa kwenye
mitandao.
Video hivyo ya sekunde 30,
inamuonyesha msichana huyo aliyekuwa kwenye shimo, akiwa amezungukwa
na wanaume waliokuwa wakimpiga mawe na uso wake ulichapwa bakora.
Msichana huyo aliyetambulika kwa
jina la Rokhshana anaumri wa kati ya miaka 19 na 21, alikuwa
akisikika akirejea kukiri imani yake ya Kiislam wakati akipigwa mawe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni