Meneja
wa mipango wa kapeni ya Binti Thamani Rosemacy Njoki akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kampeni ya kuwahamasisha
wasichana kupenda kujiunga na vyuo vya ufundi ili kujifunza ufundi
stadi na kujiendeleza kimaisha ikiwa ni pamoja na kujipatia ajira
endelevu, amesema hayo katika kutano uliofanyika leo jijini Dar es
Salaam. Kushotoni Mkuu wa Chuo cha ufundi cha Don Bosco Dodoma Fromac
Mulu.
Mratibu wa kampeni ya Binti Thamani wa taasisi ya Don Bosco, Agnes Mgongo, kisisitiza jambo katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkufunzi wa Chuo cha Ufundi cha Don Bosco Jose Kaippan.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja wa mipango wa kapeni Binti Thamani Rosemacy Njoki
Wafanyakazi wa Taasisi ya Don Bosco wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chuo cha ufundi cha Don Bosco.
Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
TAASISI
ya kidini ya Don Bosco imeandaa kampeni ya kuwahamasisha wasichana
kupenda kujiunga na vyuo vya ufundi ili kujifunza ufundi stadi na
kujiendeleza kimaisha ikiwa ni pamoja na kujipatia ajira endelevu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Meneja wa mipango wa kapeni ya Binti Thamani, Rosemacy Njoki amesema
wana vyuo mbalimbali hapa nchini ambavyo vinatoa mafunzo ya ufundi
stadi kwa vijana lakini kumekuwa na asilimia ndogo ya vijana wakike
wanaojiunga na mafunzo ya ufundi stadi ukilinganisha na idadi ya vijana
wa kiume kwa mwaka.
amesema
baadhi ya kozi zinazotolewa na vyuo vya Don Bosco vilivyopo Dar es
Salaam Dodoma na Iringa ni ufundi Seremala, uchongaji vipuri, uungaji
na uundaji vyuma, umeme wa viwandani na majumbani, uhazili, ujenzi,
ufundi bomba na magari, ufundi cherehani uchapishaji na kompyuta.
Kampeni
ya Binti thamani ni mwendelezo wa uhamasishaji kwa wasichana kuibua na
kutatua changamoto mbalimbali za vijana hususani wasichana kutambua kuwa
kuna fursa ya kujiendeleza na kufanikiwa kupitia mafunzo ya ufundi
baada ya kumaliza mafunzo yao.
Kampeni hiyo itasaidia kuwakumbusha kuwa wasichana nao wana uwezo wa kufanya kazi yoyote hasa anapokuwa na malengo chanya.
Kampeni
hiyo leo itawakutanisha wasichana mbalimbali hasa wanafunzi wa shule za
sekondari wapatao 1000 katika mikoa wa Dar es Salaam.
“Lengo
la kampeni hii ni kuwakutanisha wasichana na wadau mbalimbali
waliopitia mafunzo ya ufundi stadi na kuwahimiza kuwa mabalozi wazuri
katika kuhakikisha wasichana wengi Zaidi wanapenda mafunzo ya ufundi
stadi.
“Tunawaomba
wazazi na walezi tusaidiane kwa pamoja katika harakati za
kuwahamasisha wasichana kwani ndio tegemeo la jamii yetu,” Rosemacy.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni