Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitia
mchanga katika kaburi la marehemu Bi. Amina Abdallah Amour katika
makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar. Marehemu Bi. Amina ambaye alifariki
ghafla jana mchana, aliwahi kuwa Mbunge wa Viti maalum (CUF) katika
awamu iliyopita na baadaye kujiunga na Chama Cha ACT-Wazalendo.
Viongozi
mbali mbali wa CUF na kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe (wa tatu
kushoto) pamoja na wananchi wakiitikia dua wakati wa mazishi ya marehemu
Bi. Amina Abdallah Amour katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar.
Kiongozi
wa ACT- Wazalendo Bw. Zitto Kabwe, akitia mchanga katika kaburi la
marehemu Bi. Amina Abdallah Amour katika makaburi ya Mwanakwerekwe
Zanzibar wakati akishiriki mazishi hayo.
Viongozi mbali mbali wa CUF na kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe pamoja na wananchi wakishiriki mazishi hayo.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na
kiongozi wa ACT- Wazalendo Zitto Kabwe, wakiwa katika makaburi ya
Mwanakwerekwe Zanzibar kushiriki mazishi hayo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akiagana na kiongozi wa ACT- Wazalendo Zitto Kabwe, baada ya kushiriki mazishi ya Mbunge huyo mstaafu wa CUF.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni