Wanawake nchini Ireland wamekuwa
wakimtumia ujumbe wa twitta Waziri Mkuu wao Enda Kenny unaoelezea
siku zao za hedhi, katika kuonyesha hasira zao dhidi ya sheria kali
za kuzuia utoaji mimba.
Mchekeshaji Grainne Maguire ndiye
alianza kumtumia ujumbe wa aina hiyo Waziri Mkuu Kenny siku ya
jumatatu katika kutaka kuondolewa kifungu cha nane cha mabadiliko ya
Katiba ya Ireland.
Mabadiliko ya Katiba ya kifungu
hicho yanaruhusu kuokoa maisha ya mama pale tu ujauzito utakapotishia
uhai wa mjamzito na ni kosa kisheria kutoa mimba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni