Watu 128 wameuawa katika matukio sita tofauti ya ugaidi yaliyopangwa na magidi jijini Paris nchini nUfaransa.
Katika matukio hayo magaidi 8 wameuawa, 7 kati yao wakiwa waliojilipua kwa mabomu ya kijitoa mhanga.
Magaidi
hao pia wamefanya mashambulio hayo katika uwanja wa mpira wa miguu wa
Stade de France uliokuwa na watazamaji 80,000 waliokuwa wakifuatilia
mchezo kati ya Ufaransa na Ujerumani, na shambulio lingine limefanyika
ukumbi wa starehe kulikokuwa na tamasha la Rock .
Kufuatia mashambulio hayo, majengo yote ya umma yamefungwa jijini Paris, shule pamoja na usafiri wa umma pia umesitishwa.
Rais wa
Ufaransa, Francois Hollande amaetangaza hali ya hatari, na baadhi ya
mipaka ya wilaya imefungwa. Viongozi wa mataifa mbalimbali duniani
wameahidi kuisaidia Ufaransa kukabiliana na ugaidi.
Watazamaji waliokuwa wakifuatilia mchezo kati ya Ufaransa na Ujerumani
wakiwa wamejazana katikati ya uwanja huo wa Stade de France baada ya
kutokeo kwa shambulio la kigaidi katika uwanja huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni