WAJUMBE wa Bodi ya barabara Zanzibar wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Mhe: Tahir Abdalla mwenye
suti na kutia mkono mfukoni, wakishuka gari na kukagua eneo ambalo
Wizara hiyo Pemba imelifukia kwa mawe kwa ajili ya kuzuwia barabara
kuliwa na maji ya mvua, karibu na kituo cha Polisi Mkoani.(Picha na Abdi
Suleiman, PEMBA.)
MHANDISI
Mkaazi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Pemba Khamis Massoud,
akitoa maenelezo kwa wajumbe wa bodi ya barabara kutoka wizara hiyo,
wakati walipofika kukagua shimo lenye urefu wa mita 15 lililofukiwa kwa
mawe karibu na kituo cha Polisi Mkoani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAFANYAKAZI wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Pemba, wakipanga
mawe katika shimo hilo lenye urefu wa mita 15 ambalo limegharimu zaidi
ya gari 200 za mawe, katibu na kituo cha polisi Mkoani.(Picha na Abdi
Suleiman, PEMBA.)
MWENYEKITI
wa Bodi ya Mfuko wa barabara Zanzibar Mwalim Haji Ameir, akimuonesha
mmoja wa mjumbe wa bodi hiyo njia ambayo maji ya mvua hupitia na
kusababisha kuvubuka kwa shimo kubwa pambeni ya barabara katibu na kituo
cha Polisi Mkoani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni