MKUU WA MKOA KILIMANJARO, AMOS MAKALLA AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA WAFUNGWA WA GEREZA LA KARANGA


Katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo yenye thamani ya shilingi milioni tatu na nusu aliwakumbusha wafungwa na mahabusu kuwa michezo hujenga umoja, michezo ni burudani, michezo ni kwa afya na zaidi kwa wenye vipaji michezo itumike kulinda vipaji vyao na siku wakitoka waviendeleze vipaji.
 
Vifaa alivyokabidhi ni pamoja na nyavu za magoli, vikombe 2 vya kushindaniwa,jezi kwa timu 5 za wafungwa na mahabusu, mipira 10 kwa ajili ya wafungwa na mahabusu, jezi moja na mpira mmoja kwa ajili ya timu ya netball ya wafungwa wanawake na jezi moja , mipira 3 na nyavu za magoili kwa ajili ya timu ya askari magereza

Uongozi wa gereza, wafungwa na mahabusu wamemshukuru sana mkuu wa mkoa kwa msaada huo na wamemuhaidi kumuenzi na kila mwaka watakuwa na ligi itakayoitwa Makalla Cup na wamewataka viongozi na wadau wengine kite nchini kuiga mfano alioonyesha mkuu wa mkoa wa kilimanjaro

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni