SERIKALI MKOANI ARUSHA YAUNDA TUME KUCHUZA BEI ZA BIDHAA KUPANDA

 Image result for felix ntibenda kijiko
 Na Mahmoud Ahmad Arusha
MKUU wa mkoa wa Arusha , Felix Ntibenda ameunda tume ya kufuatilia
upandaji holela wa bidhaa za chakula unaofanywa na baadhi ya
wafanyabiashara jijini hapa ambao umepekelea kuwepo kwa malalamiko
mbalimbali kutoka kwa wananchi.

Aidha bidhaa zilizopanda ni pamoja na nyama ambapo hapo awali kilo
mmoja ilikuwa shs 3,000 kwa sasa imefika 4,000 ambapo bei hizo
zimepanda kiholela bila kuwepo kwa sababu zozote za msingi.

Ntibenda alisema kuwa, ameunda tume ya kuchunguza swala hilo ambapo
wafanyabiashara watakaobainika kupandisha bei hizo kiholela
watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufutiwa leseni zao mara
moja.

‘mimi malalamiko haya nimeyapata kutoka kwa wananchi mbalimbali kuwa
bidhaa zimepanda mara dufu na bei hizo ni kuanzia apatikane Rais wa
jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dokta  John Pombe Magufuli ambapo
wafanyabiashara hao wamekuwa wakiwakebei wateja kuwa nyie mmechagua
CCM sasa mtaona cha moto’alisema Ntibenda.

Aliongeza kuwa,bei hizo zimekuwa zikipandishwa kiholela na baadhi ya
vikundi vyenye lengo la kudhalilisha uongozi mpya uliopo madarakani
,hatua ambayo alisema mara moja watakaobainika kuendeleza zoezi hilo
leseni zao zitafutiwa mara moja .

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi ,Mariam Juma mkazi
wa Mbauda alisema kuwa, wanashangazwa na kitendo cha bidhaa kupanda
bei  kiholela bila wao kupata taarifa zozote  kitendo  ambacho
kinawaathiri sana wananchi walio wengi.

Abdalah Husein mkazi wa Ngarenaro alisema kuwa, bidhaa mbalimbali za
vyakula zimepanda bei tangu kupatikana kwa Rais mpya ,kwa madai kuwa
wananchi ndo wamechagua kiongozi wa CCM hivyo ndivyo mambo
yatakavyokuwa.

‘jamani tunaomba sana mamlaka husika watusaidie kuingilia kati suala
hili kwani haiwezekani watukomoe kwa sababu ya kumchagua kiongozi wa
mpya wa CCM ,hali inakuwa ngumu sana kwani kila kitu kimepanda bei
unakuta kitu kilikuwa kinauzwa 1,000 sasa hivi ni 2,000 tunaomba sana
vyombo husika wafanye kazi yake kutunusuru na hali hii’alisema
Abdalah.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni