ILE KUSINZIA BAR TU, AKACHORWA MIWANI USONI MWAKE


Kidume mmoja mwenye tabia ya kulala kila anapozidiwa na kilevi huko Swansea nchini Uingereza, amepewa dawa ya kutosinzia wala kulala tena kwenye baa pale anapokuwa amelewa.

Dawa aliyopewa kidume huyo na rafiki zake, ni kuchorwa tatoo ya miwani aina ya Ray-Ban kwa wino maalumu wa kuchorea tatoo ambao haufutiki kwa sabuni wala dawa nyepesi za kuondoa michoro mwilini.

Kabla ya kadhia hiyo, ambayo imemfanya njemba huyo kupandwa na hasira na kumtafuta kisirisiri rafiki yake aliyemchora tatoo hiyo, jemba huyo na rafiki zake walitoka na kwenda kwenye baa moja ili kupata kilevi cha jioni.

Ni baada ya kupata glasi mbili tatu za kilevi ndipo kidume huyo kama kawaida akapitiwa na usingizi na hapo mmoja wa rafiki zake akaamua kumchora tatoo ya miwani ya Ray-Ban usoni na kumfanya aonekane kama aliyevaa miwani.

Ilibidi kidume huyo atumie kiasi kikubwa cha fedha ili kuondoa wino wa tatuu hiyo kwenye kliniki moja ya urembo huko Swansea na sasa ameacha kunywa na kundi la marafiki huku akimtafuta kimyakimya rafiki aliyemchora tatoo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni