SERIKALI YALIFUTA GAZETI LA MAWIO

nape1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (mwenye suti ya kijivu) akiwaeleza Waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya Uamuzi wa Serikali wa kulifuta Gazeti la MAWIO katika Daftari la Msajili wa Magazeti mara alipokutana na waandishi hao 17 Januari 2016 katika Ukumbi wa Idara ya Habari uliopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene, wa pili kulia ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia usajili wa Magazeti, Bw. Raphael Hokororo na anayemfuatia ni Mwanasheria wa Wizara Bw. Patrick Kipangula
nape2
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa ya Serikali toka kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (hayupo pichani) juu ya Uamuzi wa Serikali wa kulifuta Gazeti la MAWIO katika Daftari la Msajili wa Magazeti mara alipokutana na waandishi hao 17 Januari 2016 katika Ukumbi wa Idara ya Habari uliopo jijini Dar es Salaam.
 
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)
………………………………………………………………………………………………..
Na Benedict Liwenga-Maelezo.
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kulifuta kutoka katika Daftari la usajili wa magazeti, gazeti lijulikanalo kama “MAWIO”.
 
Amri ya kulifuta Gazeti hilo imetolewa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye wakati alipokutana na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) uliopo Jijini Dar es Salaam.
 
Mhe. Nnauye amesema kuwa kupitia Tangazo la Serikali Na. 55 lililotolewa tarehe 15 Januari, 2016 Serikali imelifuta Gazeti hilo ikiwa ni uamuzi uliotolewa kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti Sura ya 229, kifungu 25(1).
 
Alieleza kuwa, hatua ya kulifuta gazeti hilo inazuia pia gazeti la Mawio kuchapishwa katika njia nyingine yoyote ikiwa ni pamoja na mitandao (Online publication) kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta Sura ya 306.
 
‘’Serikali kwa masikitiko makubwa, imechukua uamuzi huu kutokana na mwenendo wa uandishi wa gazeti hilo usioridhisha wa kuandika na kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na kuhatarisha amani, utulivu na usalama wa nchi yetu’’, alisema Nnauye.
 
Aidha, alifafanua kuwa hatua hiyo ya kulifuta gazeti hilo imechukuliwa baada ya Msajili wa Magazeti kufanya juhudi kubwa za muda mrefu kuanzia Juni, 2013 hadi Januari,  2016  kumtaka Mhariri wa gazeti hilo kubadili aina ya uandishi wa habari na makala katika gazeti lake, bila mafanikio.
 
‘’Msajili wa magazeti kwa juhudi zake alifanya mawasiliano na Mhariri wa gazeti hilo mara nane kwa lengo la kutaka afanye marekebisho ya  mtindo wa kutoa habari zake lakini mhariri wa gazeti hilo hakuzingatia ushauri mzuri aliopewa na Msajili wa Magazeti,
Ninatoa wito kwa wamiliki, wahariri, waandishi na watangazaji wa habari kuzingatia sheria, Kanuni na taratibu za taaluma ya uandishi wa habari ambazo zikizingatiwa hakutakuwa na migogoro yoyote. Aidha Serikali inasisitiza kwamba inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari unaozingatia maadili, weledi na Sheria za nchi na kwamba Serikali itaendelea kushirikiana navyo’’ alisisitiza Mhe. Nnauye.
 
Katika hatua nyingine, Waziri nape alitoa pongezi kwa Vyombo vyote vya habari nchini vinavyozingatia maadili, weledi na Sheria zinazosimamia taaluma ya habari na sheria nyingine za nchi. 
 
‘’Kwa namna ya pekee Serikali inawapongeza wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari ambavyo vinapofanya makosa vikielekezwa hujirekebisha na kutoa ushirikiano kwa Serikali na pia kubadili mwenendo wao; hawa ni pamoja  na wahariri wa magazeti ya; Mwananchi Tanzania, Mtanzania, The East African, Magazeti ya Daily News na Habari Leo, Uhuru na mengineyo’’, alisema Mhe. Nnauye.

Nape akutana na Balozi wa Israel nchini na kukubaliana kushirikiana katika sekta za Habari na Utamaduni

pe1
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(kulia) akifurahia jambo na Balozi wa Israel nchini Tanzania Bw.Yahel Vilan alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.Katika maongezo yao wamekubaliana kuimarisha ushirikiano uliokuwepo na kuangalia sehemu zaidi za kushirikiana katika sekta za Habari na Utamaduni.
pe2
Balozi wa Israel nchini Tanzania Bw.Yahel Vilan(kushoto) akimpongeza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Nape Nnauye(kulia) kwa kuchaguliwa kuwa Waziri  pamoja na kumpatia zawadi ya kitabu na kikombe kutoka Israel alipomtembelea leo jijini Dar es Salaam.
pe3
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Nape Nnauye(kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Israel nchini Tanzania Bw.Yahel Vilan(kulia) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

WAZIRI NAPE:HONGERA SANA BWANA MICHUZI KWA KUWA MWENYEKITI WA FK


mwenyekiti
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (mwenye suti ya kijivu) akimpongeza mwenyekiti mpya wa FK aliyeteuliwa hivi karibuni Bw. Ahmed Michuzi ambaye pia ni Mmiliki  wa Blogu ya Jiachie na mkurugenzi mwandamzi  wa Michuzi  Michuzi Media alikuwa mwanachama mwaminifu wa FK, tukio hilo limetokea leo wakati alipokutana naye kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo  jijini Dar es salaam, Cheo hicho kilikuwa kikishikiliwa na Kamanda Richard Mwaikenda.

WALIONYIMWA HIFADHI YA UKIMBIZI NCHINI KENYA KUREJESHWA BURUNDI JANUARY 16


ARUSHAMahmoud Ahmad Arusha
…………………………………….
IDARA ya Uhamiaji mkoa wa Arusha, January 16 inawarejesha kwenye kambi ya wakimbizi raia wa Burundi 21 ,akiwemo mwanamke mtanzania,walionyimwa hadhi ya ukimbizi nchini Kenya..
Afisa Uhamiaji mkoa wa Arusha, Ndelema Mwakipesile, alisema hayo ofisini kwake kuwa wakimbizi hao akiwemo mwanamke mtanzania ambae ameolewa na raia wa Burundi, walikataliwa kuingia nchini Kenya kutokana na kutokuwa na sifa za ukimbizi.
Mwakipesile,alisema raia hao wa Burundi, waliingia nchini wakipitia mpaka wa Kabanga uliopo mkoani Kigoma na kudai wamekuja kuwatembelea ndugu zao lakini mara baada ya kuingia nchini walibadirisha mawazo na kuamua kwenda nchini Kenya kutafuta hifadhi kwenye kambi ya Kakuma nchini Kenya.
Raia hao 21 wakiwemo watoto 14 walipofika mpakani Namanga wakitaka kuingia nchini humo walidai wanatafuta hifadhi ya ukimbizi na serikali ya Kenya iliwazuia na kuwarejesha Tanzania ,ambako ndiko walikopitia kuelekea Kenya.
Mwakipesile, alisema cha kushangaza raia hao wa Burundi kila mmoja ana hati ya kusafiria jambo ambalo linaonyesha walikuwa wamejiandaa kwa kuwa sheria za kimataifa za ukimbizi haziruhusu mkimbizi kuwa na hati bali mkimbizi anakuwa na vitu vichache tu pia mkimbizi hachagui kambi ya kupelekwa .
Alisema walipoulizwa kulikoni waende Kenya, wakimbizi wamesema kuwa wamekuwa wakiingia nchini mara kwa mara kwenye kambi ya wakimbizi ya Kibondo,na wamekuwa wakirejeshwa kwao mara kwa mara wanapoingia nchini.
Mwakipesile, alisema wakimbizi hao hataki kurejeshwa kwao sasa wamebadirisha mawazo na kuamua kutafuta hifadhi nchini Kenya ili kukwepa kurejeshwa kwao.
Alisema wanarejeshwa makwao kwa kuwa hawana kosa lolote kwa mjuibu wa taratibu za kimataifa hivyo watapelekwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Kibondo, ili wasubiri taratibu zingine .
Mwakipesile alisema kulingana na sheria mkimbizi hawezi kuomba nchi ya kwenda, pia haruhusiwi kwenda nchi ya tatu kutoka kwao bali anatakiwa kukimbilia nchi wanayopakana nayo
Raia hao wa Burundi, walikutwa ndani ya Basi la Tahmeed Coach, lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Nairobi nchini Kenya na walipofika mpaka wa Namanga, wakazuiliwa kuingia nchini Kenya .
Rai mmoja wa Burundi,ambae hakutaka jina lake liandikwe kwa sababu ya usalama ,ambae ni dereva wa malori,amesema wamekuwa wakiingia nchini mara kwa mara kwenye kambi ya wakimbizi na wamekuwa wakirejeshwa kwao sasa wanataka kwenda kuishi kwenye kambi iliyo mbali na kwao kwa kuhofia usalama wao.
Alisema mwezi Desemba mwaka jana akiwa nyumbani kwake nchini Burundi,watu watatu waliuliwa mbele ya nyumba yake na watoto wake wamekuwa wakiogopa kuishi kutokana na kutokuwepo amani nchini mwao na hiyo ni sababu ya msingi ya kuomba ukimbizi.
Alisema kuwa yeye amekuwa ni dereva wa malori kwa miaka 20 amekuwa akisafirisha mizigo kata ya Tanzania na Burundi, lakini kutokana na ukosefu amani nchini mwao ameamua kikimbia kutafuta hadhi ya ukimbizi nchini Kenya.
Alisema Tanzania anaipapenda tatizo ni kuwa Tanzania imekuwa ikiwarudisha mara kwa mara nchini Burundi hivyo wanaomba kwenda nchi ya mbali ili wasirudishwee mwakwao.
Ameongeza kuwa maafisa wa Burundi wamekuwa wakienda kwenye kambi ya wakimbizi na kuwatambua na kasha huuliwa hivyo wanahofia usalama wao.
Kwa upande wake Mtanzania aliyeolewa na raia huyo wa Burundi, Eva Michael Magumula,(37) mzaliwa wa Dodoma, alisema ana watoto 6 inalazimika aambatane na mume wake ili waweze kulea familia yao.

T.I.B YAKUBALI KUTOA FEDHA UJENZI WA HOSPITALI ARUSHA


ARUSHANa Mahmoud Ahmad Arusha
………………………………………
BENKI ya uwekezaji nchini TIB, imekubali kutoa shilingi bilioni 31 kugharimia ujenzi wa hospital ya rufaa ya mkoa wa Arusha, ambayo itajengwa kwenye eneo la hospital ya mkoa ya Mount Meru mapema mwaka huu.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, amesema kuwa tayari taratibu za kupatikana kwa fedha hizo ambazo ni mkopo zimekamilika na hivi karibuni kutasainiwa mkataba kati ya benki hiyo na ofisi ya katibu tawala mkoa ili ujenzi huo uweze kuanza mara moja.
Ntibenda, amesema mkoa unaendelea wa kuboresha,majengo na huduma ya afya kwenye hospital hiyo ya mkoa wakati wakisubiri hospital ya rufaa ijengwe.
Amesema,ukarabati wa hospital hiyo unaofanywa kwa kushirikiana na wadau umewezesha kuirejesha hadhi ya hospital hiyo.
Amesema kuwa mkoa umewezesha kuanzishwa kwa bohari la dawa la MSD,ambalo tayari maandalizi yamefikia 95% na itafunguliwa wakati wowote na kuanza kutoa huduma za dawa kwa bei nafuu zaidi kuliko zinavyouzwa kwenye maduka binafsi.
Kwa upande wake,Katibu tawala mkoa wa Arusha, Adoh Mapunda, amesema kuwa wiki ijayo mkoa utasaini makubaliano ya kupatiwa mkopo na benki hiyo na kufuatiwa na hatua ya kutangaza zabuni ili kumpata mkandarasi atakae jenga hospital hiyo yenye majengo ya ghorofa tano ya hospital hiyo ya rufaa.
Amewapongeza wadau ambao wamejitokeza kuchangia ukarabati wa hospital hiyo ya mkoa unaoendelea na tayari jengo la wadi ya Grade one ,ambalo lilikuwa likihudumia kulaza wagonjwa katika hospital hiyo ya mkoa limefungwa likisubiri kubomolewa kutokana na uchakavu.
Akiwasilisha mpango kazi na mchoro wa jengo hilo, Mhandisi wa mkoa, Edward Amboka ,amesema kuwa hospital hiyo iliyojengwa mwaka 1915 majengo yake yamechakaa sana na hayafai kuendelea kutumika kama hospital .
Hospital hiyo ilijengwa ikiwa ni kambi ya kutibia majeruhi wa vita ya kwanza ya dunia hivyo mpango uliopo ni kujenga majengo mapya ya ghorofa na kubomoa ya zamani ambayo yamechakaa.
Amesema ujenzi huo utahusisha maeneo manane zikiwemo nyumba za watumishi ,mafunzo, mapumziko na maegesho ya magari.na mipango mingine ya uendelezaji wa hospitali hiyo
Amesema lengo la kujenga majengo hayo ni kupunguza mzigo wa wagonjwa mkoani Arusha ikiwemo vizazi na vifo vinavyotokana wakati wa kujifungua hivyo wanajenga jengo moja la ghorofa tano ambalo litatosheleza mahitaji badala ya kuwa na utitiri wa majengo
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospital hiyo, Dakta Jacklin Urio, amesema hospital hiyo ina vitanda 500 na ina hudumia watu milioni 1.6 kwa mwaka lakini kutokana na ukuaji wa mji na ongezeko la watu hospital hiyo kwa sasa haitoshelezi mahitaji kutokana na wingi wa watu.
Amesema kuwa ujenzi wa hospital mpya ya rufaa utaiwezesha hospital ya rufaa kuwa na vitanda 600 ,kutakuwa ni vitanda 50 kwa ajili ya wagonjwa mahututi, ICU, na kati yake vitatu ni kwa ajili ya watu maalumu (VIP) wakiwemo viongozi wa kitaifa na kimataifa .
Jengo la Grade A,lilikuwa na vitanda 6,lakini kwa sasa halikidhi mahitaji na jengo jipya litakuwa na maabara ,wataalam, vitanda 50 vya wagonjwa wa Mahututi,(ICU) na huduma zingine .

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Atembelea Idara ya Uhamiaji Zanzibar.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Hamad Masauni, akisalimiana na Maofisa wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar wakati wa ziara yake kutembelea Idara hiyo ya Uhamiaji Zanzibar.kushoto Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Hamad Masauni, akisalimiana na Maofisa wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar wakati wa ziara yake kutembelea Idara hiyo ya Uhamiaji Zanzibar.Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Hamad Yussuf Masauni akipata maelezo kutoka kwa Afisi wa Uhamiaji Zanzibar wakati wa ziara yake katika Idara ya Uhamiaji Zanzibar. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mhe Hamad Yussuf Masauni akitembelea Vitengo vya Idara ya Uhamiaji Zanzibar wakati wa ziara yake na kuangalia Utendaji wa Idara hiyo Zanzibar.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani akimsikiliza Afisa Uhamiaji Zanzibar akitowa maelezo ya jinsi ya kuweka kumbukumbu za Passport wakati wa ziara yake.
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Hamad Yussuf Masauni, wakati wa ziara yake katika Idara hiyo Zanzibar. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mhe Hamad Yussuf Masauni akizungumza na Maofisa wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar baada ya ziara yake ya kujitambulisha na kuangalia ufanisi wa kazi za Idara hiyo Zanzibar.
Maofisa wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Eng Hamad Yussuf Masauni akizungumza na Maofisa hao baada ya ziara yake kutembelea Idara hiyo kuina ufanisi wa Kazi zake kwa Wananchi wanaofika kupata Passport.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot
Zanzinews.com

WAZIRI MBARAWA AWATAKA MAKANDARASI MKOANI MTWARA KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA KWA WAKATI.


Z1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa akiweka saini kwenye kitabu cha kumbukumbu mara alipowasili Mkoani Lindi kwa Ziara ya Kukagua miradi inayotekelezwa na Wizara hiyo.Kulia ni ni Bi.Mariam Mtima Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa.
Z2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa akipokea taarifa ya Ujenzi wa barabara ya Mangaka-Mtambaswala (KM 62.7), kutoka kwa Mhandisi Mkazi Anold Msengezi (Katikati) anayesimamia ujenzi wa barabara hiyo.
Z3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo juu ya Ujenzi wa barabara ya Mangaka-Mtambaswala (KM 62.7), ambapo amemtaka Mkandarasi kukamilisha Ujenzi huo kwa wakati na ubora unaokusudiwa.
Z4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia) akipokea taarifa ya Ujenzi wa barabara ya Mangaka –Nakapanya (KM70.5) kutoka kwa Mhandisi mkazi Dkt.Chaurasia inayojengwa na kampuni ya Jiangxi Geo Engineering (Group) Cooperation ya China.
Z5
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na wakazi wa Nakapanya alipopita kukagua bujenzi wa barabara ya Mangaka-Mtambaswala (KM 62.5).
Z6
Sehemu ya barabara ya Mangaka –Mtambaswala (KM 62.5) ambayo Ujenzi wake unaendelea kwa kiwango cha lami.
Z7
Tingatinga likiwa linaendela na kazi za ujenzi barabara ya Mangaka –Mtambaswala (KM 62.5) ambayo Ujenzi wake unaendelea kwa kiwango cha lami.
…………………………………………………………………………
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amewataka makandarasi wanaojenga barabara za Mangaka-Mtambaswala KM 62.7 na Mangaka-Nakapanya Km 70,5 kukamilisha ujenzi huo ifikapo Juni mwaka huu.
Amewataka makandarasi hao kuongeza rasilimali watu na vifaa ili ujenzi huo ukamilike kama ilivyopangwa katika mkataba wa ujenzi wake.
“Hakuna muda utakaoongezwa nataka miradi yote miwili iwe imekamilika ifikapo juni mwaka huu tena iwe kwenye ubora unaowiana na thamani ya fedha,”amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Barabara hizo ambazo ujenzi wake kwa kiwango cha lami ulianza mwaka 2014 zitafungua fursa za kiuchumi mkoani Mtwara ikiwemo kuiunganisha Tanzania na Msumbiji kwa lami kupitia daraja la umoja lililoko Mtambaswala.
Akizungumza katika ziara hiyo Meneja wa Wakala wa Barabara TANROADS mkoa wa Mtwara Eng. AISHA SALIM amesema hawata kubali maombi yoyote ya kuongeza muda wa ujenzi wa barabara hizo ambapo ujenzi wa barabara ya Mangaka –Mtambaswala Km 62.7 unatarajiwa kukamilika mwezi Mei na ule wa Mangaka-Nakapanya KM 70.5 ukitarajiwa kukamilika mwezi julai mwaka huu.
Mapema Prof. Mbarawa alikagua hali ya barabara wilayani Ruangwa,Nachingwea na Masasi na kusisitiza kuwa ujenzi wa barabara na madaraja katika wilaya hizo utaendelea katika kipindi kifupi baada ya Serikali kuanza kutoa fedha kwa miradi inayotumia fedha za Mfuko wa Barabara (RFB).
Waziri Mbarawa yuko katika ziara ya mikoa ya lindi na mtwara kukagua miradi ya Barabara,Mawasiliano na Bandari ili kuona ufanisi uliopo katika sekta hizo.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano