WALIONYIMWA HIFADHI YA UKIMBIZI NCHINI KENYA KUREJESHWA BURUNDI JANUARY 16


ARUSHAMahmoud Ahmad Arusha
…………………………………….
IDARA ya Uhamiaji mkoa wa Arusha, January 16 inawarejesha kwenye kambi ya wakimbizi raia wa Burundi 21 ,akiwemo mwanamke mtanzania,walionyimwa hadhi ya ukimbizi nchini Kenya..
Afisa Uhamiaji mkoa wa Arusha, Ndelema Mwakipesile, alisema hayo ofisini kwake kuwa wakimbizi hao akiwemo mwanamke mtanzania ambae ameolewa na raia wa Burundi, walikataliwa kuingia nchini Kenya kutokana na kutokuwa na sifa za ukimbizi.
Mwakipesile,alisema raia hao wa Burundi, waliingia nchini wakipitia mpaka wa Kabanga uliopo mkoani Kigoma na kudai wamekuja kuwatembelea ndugu zao lakini mara baada ya kuingia nchini walibadirisha mawazo na kuamua kwenda nchini Kenya kutafuta hifadhi kwenye kambi ya Kakuma nchini Kenya.
Raia hao 21 wakiwemo watoto 14 walipofika mpakani Namanga wakitaka kuingia nchini humo walidai wanatafuta hifadhi ya ukimbizi na serikali ya Kenya iliwazuia na kuwarejesha Tanzania ,ambako ndiko walikopitia kuelekea Kenya.
Mwakipesile, alisema cha kushangaza raia hao wa Burundi kila mmoja ana hati ya kusafiria jambo ambalo linaonyesha walikuwa wamejiandaa kwa kuwa sheria za kimataifa za ukimbizi haziruhusu mkimbizi kuwa na hati bali mkimbizi anakuwa na vitu vichache tu pia mkimbizi hachagui kambi ya kupelekwa .
Alisema walipoulizwa kulikoni waende Kenya, wakimbizi wamesema kuwa wamekuwa wakiingia nchini mara kwa mara kwenye kambi ya wakimbizi ya Kibondo,na wamekuwa wakirejeshwa kwao mara kwa mara wanapoingia nchini.
Mwakipesile, alisema wakimbizi hao hataki kurejeshwa kwao sasa wamebadirisha mawazo na kuamua kutafuta hifadhi nchini Kenya ili kukwepa kurejeshwa kwao.
Alisema wanarejeshwa makwao kwa kuwa hawana kosa lolote kwa mjuibu wa taratibu za kimataifa hivyo watapelekwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Kibondo, ili wasubiri taratibu zingine .
Mwakipesile alisema kulingana na sheria mkimbizi hawezi kuomba nchi ya kwenda, pia haruhusiwi kwenda nchi ya tatu kutoka kwao bali anatakiwa kukimbilia nchi wanayopakana nayo
Raia hao wa Burundi, walikutwa ndani ya Basi la Tahmeed Coach, lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Nairobi nchini Kenya na walipofika mpaka wa Namanga, wakazuiliwa kuingia nchini Kenya .
Rai mmoja wa Burundi,ambae hakutaka jina lake liandikwe kwa sababu ya usalama ,ambae ni dereva wa malori,amesema wamekuwa wakiingia nchini mara kwa mara kwenye kambi ya wakimbizi na wamekuwa wakirejeshwa kwao sasa wanataka kwenda kuishi kwenye kambi iliyo mbali na kwao kwa kuhofia usalama wao.
Alisema mwezi Desemba mwaka jana akiwa nyumbani kwake nchini Burundi,watu watatu waliuliwa mbele ya nyumba yake na watoto wake wamekuwa wakiogopa kuishi kutokana na kutokuwepo amani nchini mwao na hiyo ni sababu ya msingi ya kuomba ukimbizi.
Alisema kuwa yeye amekuwa ni dereva wa malori kwa miaka 20 amekuwa akisafirisha mizigo kata ya Tanzania na Burundi, lakini kutokana na ukosefu amani nchini mwao ameamua kikimbia kutafuta hadhi ya ukimbizi nchini Kenya.
Alisema Tanzania anaipapenda tatizo ni kuwa Tanzania imekuwa ikiwarudisha mara kwa mara nchini Burundi hivyo wanaomba kwenda nchi ya mbali ili wasirudishwee mwakwao.
Ameongeza kuwa maafisa wa Burundi wamekuwa wakienda kwenye kambi ya wakimbizi na kuwatambua na kasha huuliwa hivyo wanahofia usalama wao.
Kwa upande wake Mtanzania aliyeolewa na raia huyo wa Burundi, Eva Michael Magumula,(37) mzaliwa wa Dodoma, alisema ana watoto 6 inalazimika aambatane na mume wake ili waweze kulea familia yao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni