KARIMJEE YAKABIDHI SCHOLARSHIP KWA WASHINDI WA SAYANSI 2015, WAPAA KWENDA IRELAND


Wanafunzi John Method (kushoto) na Edwin Luguku (wa pili kulia) kutoka Shule ya Sekondari Mzumbe mkoani Morogoro wakipokea hati zao za ufadhili kutoka kwa Karimjee na Ofisa Ubalozi wa Ireland nchini, Bi. Carlo. Wanafunzi hao waliibuka washindi wa jumla katika maonesho ya Sayansi kwa Shule za Sekondari mwaka 2015 yanayoandaliwa na taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST). (Picha zote na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com).
Ofisa Ubalozi wa Ireland nchini, Bi. Carlo, akizungumza na Edwin Luguku na John Method kutoka Shule ya Sekondari Mzumbe, Morogoro ambao waliibuka washindi wa jumla katika maonesho ya Sayansi kwa Shule za Sekondari mwaka 2015 yanayoandaliwa na taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST). Wanafunzi hao wanaondoka leo hii kwenda Dublin, Ireland kwa maonesho ya sayansi.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST), Dk. Gozibert Kamugisha, akizungumza wakati wa kukabidhiwa kwa scholarship kwa wanafunzi Edwin Luguku na John Thomas wa Shule ya Sekondari Mzumbe ambao walikuwa washindi wa jumla katika maonesho ya sayansi 2015. Wanafunzi hao walipewa scholarship hizo la taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation ya jijini Dar es Salaam.
Meneja wa taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation, Devota Rubama, akizungumza kabla ya kukabidhi hati za ufadhili kwa wanafunzi Edwin Luguku na John Thomas wa Shule ya Sekondari Mzumbe, Morogoro walioshinda katika maonesho ya sayansi 2015.

          Mzee Karimjee, Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee Foundation.
Toyota Tanzania Limited nao waliwazawadia vijana hao kwa ushindi walioupata.

Na Daniel Mbega wa brotherdanny.com

TAASISI ya Karimjee Jivanjee Foundation ya jijini Dar es Salaam leo hii imekabidhi scholarship kwa wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari Mzumbe, Morogoro, ambao waliibuka washindi wa jumla katika Maonesho ya Tano ya Sayansi ya YST kwa Shule za Sekondari Tanzania Agosti 2015.

Wanafunzi hao, Edwin Luguku na John Method, ambao leo hii wanakwenda jijini Dublin, Ireland kuhudhuria Maonesho ya 53 ya Sayansi, waliibuka washindi kutokana na utafiti wao wa sayansi usemao “Madhara ya Matumizi ya Mifuko ya Plastiki Tanzania na Namna ya Kupunguza Matumizi hayo” (The Effects of Using Plastic Bags in Tanzania and How to Reduce the Same).

Kutokana na udhamini huo, wanafunzi hao wawili ambao wanatarajia kumaliza kidato cha sita mwaka huu, watasomeshwa na taasisi hiyo chuo kikuu huku wakilipiwa ada pamoja na gharama nyingine zote kwa miaka yote watakayokuwa wanachukua shahada zao.

Itakumbukwa kwamba, Taasisi ya Karimjee Jivanjee mbali ya kutoa scholarship kwa wanafunzi hao, pia ilitoa ufadhili kwa shahada ya kwanza chuo kikuu kwa wanafunzi Petro Samson Ndegeleki na Juma Joshua Wiliam kutoka Nassa Sekondari ya Simiyu ambao utafiti wao ulihusu ‘How Different Natural Fertilizers Affect the Growth Of Maize’.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni