Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, (wanne kutoka kushoto), Naibu
Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Susan Kolimba, (watatu kutoka kushoto)
wakiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki,
EALA, kutoka Tanzania, Mh. Shy-Rose Bhanji, wakwanza kushoto), Mh.
Makongoro Nyerere (wapili kushoto), Mh. Angella Kizigha, (Wasita kutoka
kushoto), naMh. Bernard Murunya). Wabunge hao walikwenda kumsalimia
waziri Mahiga na kujitambuslisha ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza
vikao vya bunge hilo jijini Arusha Januari 24, 2016. (K-VIS
MEDIA/Khalfan Said)
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, mapema leo Ijumaa Januari 15,
2016 amekutana na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka
Tanzania waliokwenda kujitambulisha na kubadilishana mawazo ofisini
kwake jijini Dar es Salaam.
Wabunge
hao waliongozwa na mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania, Mh. Makongoro
Nyerere, Mh. Shy-Rose Bhanji, Mh. Angella Kizigha, na Mh.Bernard
Murunya.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Susan Kolimbanaye alikuwepo wakatiwa kikao hicho kifupi cha kutambuana.
Akizungumza
na Waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho, Mwenyekiti wa wabunge
wa EALA kutoka Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, alisema, “Tumefika
kujitambulisha kwa Mh. Waziri kama ujuavyo yeye ni mgeni kwenye wizara
hiyo, tulikuwana Dkt. Mwakyembe na sasa tunaye Dk. Augustine Mhiga, kwa
hivyo tuliona ni vyematukafika kujitambulisha na kutambuana.” AlisemaMh.
Makongoro na kuongeza, “Lakini pia lazima utambue kuwa vikao vya EALA,
vinaanza Januari 24 pale Arusha na Mh. Mahiga ndiye mwenyekiti wa Baraza
la Mawaziri wa Afrika Mashariki, kwa hivyo sio busara tukakutanie kule
ndio maana tumeona ni vema tukaja kumsalimia hapa atutambue na
kubadilishana mawazo hapa na pale.” Alimaliza Mh. Makongoro.
Bunge
la Afrika Mashariki, EALA, ni chombo cha kutunga sheria cha Juamuiya ya
Afrika Mashariki na linaundwa na nchiwanachama wa Jumuiya hiyo
ambaonipamoja na Tanzania, inayoshikilia uenyekiti kwa sasa, Uganda,
Kenya, Rwanda na Burundi.
Dkt. Mahiga, akisaliamiana na mmoja wa wabunge hao, Mh. Shy-Rose Bhanji
Mh. Shy-Rose Bhanji akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga, (wakwanza kushoto) na maafisa wengine wa
wizara hiyo, mara baada ya kikao hicho
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Susan Kolimba, akisalimiana na Mh. Shy-Rose Bhanji |
Mh. Makongoro Nyerere, akipena mikono na Bi. Mindi Kasiga
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni