TUKAE NYONYANI :MWANAMKE DEREVA ANAYEENDESHA MAGARI YA MASAFA MAREFU

Dereva Tukae Ngonyani akiwa kwenye usukani kwenye moja ya lori la kusambaza vinywaji analoliendesha 
Dereva Tukae Ngonyani akiwa amesimama katika moja ya lori la kusambaza vinywaji analoliendesha
Dereva Tukai Ngonyani akishuka kwenye Folk Lift anayoendesha baada ya kuchapa kazi
.  Dereva Tukae Ngonyani akiendesha  Folk Lift  katika kiwanda cha TBL kilichopo Ilala jijini Dar es Salaam
********
  • Atoa ushauri kwa wanawake wenzake kuzingatia  falsafa ya ‘Hapa Kazi’

“Wanawake wa Tanzania tunakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na kukandamizwa na mfumo dume kwa muda mrefu. Moja ya changamoto kubwa ni  kuachwa nje ya mfumo wa ajira rasmi na  zisizo rasmi”.Anasema Tukae Ngonyani ambaye ni dereva wa magari makubwa ya kusambaza vinywaji ya kampuni ya Tanzania Breweries Limited katika kiwanda cha Ilala jijini Dar es Salaam.

Pamoja na ukosefu wa ajira kuwa moja ya changamoto kubwa inayowakabili wanawake ,Tukae anasema kuwa wanawake wengi nao wana tatizo la kushindwa kujiamini na kuwa na kasumba ya kuchagua kazi na kudhani kuwa baadhi ya kazi ni kwa ajili ya wanaume tu wakati hakuna kitu kama hicho.

“Inafurahisha hivi sasa akina mama wameweza kuwa na mwamko wa kufanya kazi mbalimbali zinazofanywa kwa wingi na wanaume,hata hivyo bado idadi yao ni asilimia ndogo na kuna haja ya kujitokeza  zaidi ili kupunguza idadi kubwa ya wanawake wasio na kazi.”Anasema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni