Mbunge wa Jimbo la Segerea 
kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mh. Bonna Kalua amesema kuwa hakuna 
nyumba ya mwananchi itakayobomolewa ambayo imejengwa katika umbali 
unaohitaji 
kisheria wa mita 60 kutoka mtoni.
kisheria wa mita 60 kutoka mtoni.
Mh.Kalua alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wananchi wa Karakata kwenye mkutano wa hadhara.
Aidha alitoa wito kwa wale 
ambao wamejenga ndani ya mita 60 na nyumba zao zimewekewa X 
kujiorodhesha majina yao kwa wenyeviti wa mitaa ili wamfikishiea Ofisi 
kwake kwa ajili ya kulifuatilia jambo hilo kwa ukaribu na hatimaye 
wapate haki zao.
Mh.Bonna aliwatahadharisha 
wananchi kutodanganywa na watu wanaowachangisha fedha kwa kigezo cha 
kufungua kesi mahakamani kuwa ni uongo na hawana nia nzuri kwa wananchi 
kwa sababu kesi ya bomoa bomoa tayari ilishafunguliwa kwa niaba ya nchi 
nzima. 
Aliwataka wananchi kuwa wavumilivu mpaka hapo shauri lilipo mahakamani litakapotolewa tamko .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni