Bondia Deontay Wilder ametetea taji
lake la uzito wa juu la kwa ushindi wa KO dhidi ya Artur Szpilka,
huku Tyson Fury akivamia uliongoni kutaka pambano na bondi huyo
Mmarekani.
Hii ni mara ya tatu kwa Wilder
kutetea taji lake hilo, ingawa haikuwa rahisi safari hii ambapo
alihangaika mno kuweza kumshinda Szpilka.
Hata hivyo ngumi kali ya kidevu
aliyoirusha Wilder, ilitosha kumaliza pambano hilo na kumuacha bondia
Szpilka akiwa chali na kulazimika kupatiwa msaa wa matibabu.
Bondia Szpilka akitupa ngumi ya kushoto iliyompata usoni Wilder
Wilder akiachia kombora la ngumi ya kushoto iliyompeleka chini Szpilka
Szpilka akiwa amelala chali na kupoteza fahamu baada ya kupigwa na Wilder
Bondia Tyson Fury akimpiga mkwara Deontay Wilder na kutaka kuandaliwa pambano naye
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni