Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro akizungumza baada ya hafla kuweka saini makubaliano kati ya pande mbili. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,Juma Idd akifafanua umuhimu wa ushirikiano kati ya Jiji na kampuni hiyo. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,Juma Idd(kulia) akifafanua umuhimu wa ushirikiano kati ya Jiji na kampuni hiyo,kushoto ni Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro. |
Diwani wa Kata ya Moshono ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango miji ya Jiji la Arusha,Metson Paul(kushoto) akiwa Mwanasheria na Mkurungezi wa kampuni ya Bondeni Seeds Limited. |
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Goodbless Lema akizungumza katika hafla hiyo. |
Halmashauri
ya Jiji la Arusha imesaini makubaliano na kampuni ya Bondeni Seeds
Limited kupima eneo linalomilikiwa na kampuni hiyo lenye ukubwa wa
Hekari 750 ili liwe sehemu ya Master Plan ya Jiji .
Meya
wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro amesema wameshawishika kuingia
makubaliano hayo na mwekezaji huyo ili kuwezesha wananchi kuishi kwenye
maeneo yaliyopimwa yanayoendana na hadhi ya Jiji na kulipatia mapato
yanayotokana naupimaji huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji,Juma Idd amesema wamekubaliana na
mwenye eneo hilo kulipanga na kuliendeleza kama sheria ya makazi
inavyotaka.
"Hatutaweza
kuendelea na makazi ambayo hayajapimwa kama Unga Limited ,Ngarenaro na
mengine ,Arusha ni eneo lenye umuhimu wake katika sekta ya utalii,madini
na ukizingatia hapa ndio Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki(EAC) na taasisi za kimataifa.
Amesema baada ya kusaini makubaliano utekelezaji unaanza mara moja ili kufikia malengo ya kuweka mji uliopangika.
Mbunge
wa Arusha Mjini,Goodbless Lema amewataka wananchi wenye maeneo makubwa
kushirikiana na uongozi wa Jiji ili maeneo yao yapimwe kuepusha makazi
holela na kuwataka waliojenga maeneo ya mabondeni na kwenye vyanzo vya
maji kubomoa nyumba zao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni