Baadhi ya
wafanyakazi wa Gazeti la Jambo Leo na familia zao, wakigongeana glasi
zenye vinywaji ikiwa ni ishara ya kutakiana heri wakati wa hafla ya
kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha ya Mwaka Mpya 2016, katika Mgahawa wa
City Sports Lounge, Dar es Salaam
Wafanyakazi
wa Jambo Leo na familia zao pamoja na wageni waalikwa wakiburudika kwa
muziki uliokuwa ukiporomoshwa wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye
Mgahawa wa kisasa wa City Sports Lounge, katikati ya Jiji la Dar es
Salaam.
Mhariri
wa Michezo na Burudani wa Gazeti la Staa Spoti ambalo ni gazeti dada la
Jambo Leo, Zahoro Mlanzi akigawa ‘champagne’ kwa wafanyakazi wenzake
wakati wa hafla hiyo.
Mpiga
Picha Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda (wa pili kulia),
akijadiliana jambo na wakurugenzi wa Kampuni za Jambo Concerpts Tanzania
Limited na Jambo Communication, Theophil Makunga (kushoto), Benny
Kisaka (wa pili kushoto) na Juma Pinto wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya
wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo, wakiwa na furaha wakati wa hafla
hiyo ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha Mwaka Mpya 2016, Dar es Salaam
juzi. Kutoka Kushoto ni Stellah Kessy, Magendela Hamis, Salha Mohamed,
Celina Mathew, Suleiman Msuya na Edith Msuya.
Wakipata mlo wa usiku
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto (kushoto),
akimuelezea Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda
kuwa wakati gazeti la Jambo Leo lilipoanzishwa 2009, alikuwa mfanyakazi
wa kwanza kujiunga na gazeti hilo akitokea Kampuni ya Business Times.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto (kushoto),
akimuelezea Mhariri wa Habari wa Gazeti la Jambo Leo, Said Mwishehe
kuwa wakati gazeti la Jambo Leo lilipoanzishwa 2009, alikuwa miongoni
mwa wafanyakazi wa kwanza kujiunga na gazeti hilo akitokea Kampuni ya
Business Times.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto (kushoto),
akimuelezea Mwandishi Mwandamizi wa Michezo na Burudani, Asha Kigundula
kuwa wakati gazeti la Jambo Leo lilipoanzishwa 2009, alikuwa miongoni
mwa wafanyakazi wa mwanzo kujiunga na gazeti hilo akitokea Kampuni ya
Business Times.
Mpigapicha
Mkuu wa Jambo Leo na magazeti mengine ya Staa Spoti na Jambo Brand
Tanzania, Richard Mwaikenda, akitoa shukrani wakati wa hafla hiyo/
Mfanyakazi Moi Dodo akiwa na wife wake
Champagne zikifunguliwa
Asha Kigundula akiwamiminia champagne wanahafla
Mwishehe na Kigundula wakikumbatiana kwa furaha
Sasa ni wakati wa kusakata muziki
Ni furaha tele
PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni