Mwanamuziki raia wa Canada, Celine
Dion amefiwa na kaka yake mkubwa aliyekuwa akiugua saratani, siku
chache tu kupita tangu afiwe na mumewe kwa ugonjwa wa saratani ya
koo.
Kaka huyo wa Dion, Daniel Dioni, 59,
amefariki dunia jana karibu na Jiji la Montreal huko Canada, kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa mwanamuziki huyo.
Familia ya Dion amemuelezea Daniel
Dion ambaye alikuwa ni baba wa watoto wawili kuwa ni mtu mkarimu,
asiye na mijivuno na ambaye alibarikiwa kuwa na vipaji vingi.
Mume wa Celine ambaye pia
aliwahikuwa meneja wake, Rene Angelil, 73, alifariki dunia siku ya
Alhamisi, nyumbani kwake Las Vegas, Marekani.
Celine Dion akiwa amekumbatiana na mumewe marehemu Rene Angelil
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni