WANAFUNZI
 538 wa chuo cha Mamlaka ya Mapato (TRA) wametunukiwa vyeti vyao leo 
katika mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa 
mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Pia wahitimu hao wameaswa kuwa waadilifu katika kazi zao kwani taaluma yao ni ukusanyaji wa mapato ya sehemu zao za kazi.
Wameaswa hayo na  Naibu
 waziri wa Fedha na Mipamgo, Ashatu Kijaji wakati akizungumza na 
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa mahafali ya nane 
ya chuo cha Mamlaka ya Mapato (TRA) yaliyofanyika katika ukumbi wa 
mikutano wa Mwalimu Nyerere.
amesema
 kuwa wahitimu wa chuo hicho wafanye kazi kwa weredi na uaminifu  kwani 
wasipofanya hiyo hawataweza kufanya kazi hayo vile inavyopaswa.
Chuo 
cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kitajengwa kingine huko  kibaha 
mkoani pwani ili kuongeza wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri kwani
 chuo kilichopo Mwenge kimezungukwa na viwanda.
 Naibu
 waziri wa Fedha na Mipamgo, Ashatu Kijaji akizumgumza na wahitimu wa 
chuo cha Mamlaka ya mapato Tanzania TRA leo katika mahafali ya nane ya 
chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere 
leo jijini Dar es Salaam
 Baadhi
 ya wahitimu wa chuo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwa katika 
mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Makamu Mkuu wa Chuo, Lewis Ishemoi akiwaita majina wanafunzi wa Mamlaka
 ya Mapato Tanzania (TRA) leo katika mahafali ya nane ya chuo hicho 
ikiwa wahitimu 538 wamehitimu mafunzo yao katika chuo hicho jijini Dar 
es Salaam leo.
Wanafunzi
 wakivaa kofia zao mara baada ya kutunukiwa katika mahafali yaliyofanika
 katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Wanafunzi
 wakivaa kofia zao mara baada ya kutunukiwa katika mahafali yaliyofanika
 katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
 Naibu
 waziri wa Fedha na Mipamgo, Ashatu Kijaji akiwatunukia vyeti wanafunzi 
waliofanya vizuri katika masomo yao katika mahafali yaliyofanyika katika
 ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
 Wahadhiri
 wakiwitunukiwa vyeti pamoja na zawadi mbalimbali katika mahafali ya 
nane ya chuo cha mamlaka ya mapato (TRA) leo jijini Dar es Salaam. 
kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Alphayo 
Kidata na Makamu Mkuu wa Chuo, Lewis Ishemoi.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.















Hakuna maoni:
Chapisha Maoni