Bondia David Haye amerejea kwa
kishindo uliongoni baada ya kupumzika kwa muda wa miaka mitatu na
nusu, kwa kumdunda kwa KO, Mark de Mori katika pambano lililofanyika
Jijini London.
Bondia Muastralia De Mori alionekana
kuchanganyikiwa mapena na ngumi ya kwanza aliyoirusha Haye na baada
ya hapo aliishia kuonekana kuwa ameelemewa.
David Haye, 35, alimaliza pambano
hilo kwa ngumi nzito ya mkono wa kulia ambayo ilimfanya De Mori
kupoteza fahamu na kuanguka chini ikiwa zimebakia dakika 49 katika
raundi ya kwanza ya mpambano huo.
Bondia David Haye akimtandika ngumi ya kichwani Mark de Mori
Ngumi nzito ya Haye iliyomuingia barabara de Mori na kupata kizunguzungu
David Haye akimalizi kazi kwa ngumi iliyompeleka chini de Mori
Haye aliyepandwa na mzuka akizuiwa na refa asije akauwa mtu ulingoni
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni