Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeanza kusikiliza Kesi ya Kupinga Matokeo
 ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Novemba 25 mwaka jana katika Jimbo la 
Bunda Mjini, Mkoani Mara ambapo Mgombea kutoka Chama cha Demokrasia na 
Maendeleo Chadema Esther Bulaya aliibuka mshindi.
Jaji wa 
Mahakama hiyo Mhe.Mohamed Gwae ameahirisha kesi hiyo hadi jumatatu ijayo
 ya Januari 25 mwaka huu baada ya mawakili wa pande zote mbili kuchuana 
vikali kwa muda mrefu. 
Waleta 
maombi (Mlalamikaji) katika kesi hiyo wametajwa kuwa ni wapiga kura wa 
jimbo hilo la Bunda Mjini ambao walikuwa wakiiomba Mahakama kutengua 
matokeo ya uchaguzi huo katika jimbo hilo kutokana na uchaguzi huo 
kukumbwa na kasoro mbalimbali ikiwemo uchaguzi kutokuwa huru pamoja na 
idadi ya wapiga kura kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika 
daftari la kudumu la wapiga kura.
Madai 
hayo yamepingwa na upande wa Mjibu Maombi (Walalamikiwa ambao ni Mbunge 
wa Jimbo la Bunda Mjini pamoja na Mwanzasheria wa Serikali) uliokuwa 
ukiongozwa na Wakili Tundu Lisu. Upande wa Mleta maombi ulikuwa 
ukiongozwa na Wakili Constantine Mutalemwa.
Kesi hiyo
 ilianza kusikilizwa majira ya saa tatu asubuhi na baadae kuahilishwa 
kwa ajili ya chakula cha mchana na kisha kuendelea kusikilizwa kuanzia 
majira ya saa nane mchana hadi majira ya saa kumi na moja jioni.
Wakili
 upande wa mjibu maombi Tundu Lisu (mwenye miwani) akizungumza baada ya 
Kesi hiyo kuahirishwa ambapo amesema hoja za waleta maombi hazina 
mashiko kwani katika hati yao ya madai hawajalalamika kuonesha kama haki
 yao imekiukwa hivyo ni vyema mahakama ikatupilia mbali maombi yao kwani
 yanaonyesha kuwa yanampigania Steven Wasira (aliekuwa mgombea ubunge 
kutoka CCM Steven Wasira) ambae hata hivyo hakuwemo mahakamani hapo.
Wakili Tundu Lisu (mwenye miwani) akizungumza baada ya Kesi hiyo kuahirishwa
Wakili
 upande wa mleta maombi, Constantine Mutalemwa (mwenye miwani) 
akizungumza baada ya kesi hiyo kuahilishwa ambapo amesema kuwa waleta 
maombi wanasubiri maamuzi yatakayotolewa na mahakama hiyo baada ya hii 
leo kuahirishwa.
Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya (Chadema)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni