Adhabu ya kifo kwa sheikh wa Kishia na watu 46 yatekelezwa

audi Arabia Jumamosi (02.01.2016) imetekeleza adhabu ya kifo dhidi ya sheikh mashuhuri wa Kishia na wanachama kadhaa wa kundi la Al Qaeda kwa makosa yanayohusina na ugaidi.

Sheikh Nimr al-Nimr pichani.
Sheikh Nimr al-Nimr pichani.
Waislamu wengi wa madhehebu ya Shia wameandamana katika kitongoji cha Qatif kilioko katika jimbo la mashariki nchini Saudi Arabia kupinga kuuliwa kwa sheikh Nimr-al-Nimr kauli mbiu ya maandamano ikilaani Al-Saudi jina la ukoo wa kifalme uaoitawala nchi hiyo.
Lakini wengi waliouliwa katika utekelazaji mkubwa kabisa wa adhabu ya kifo kwa pamoja kuwahi kushuhudiwa kwa miongo mingi nchini humo walikuwa Wasuni waliopatikana na hatia ya mashambulizi ya kundi la Al Qaeda nchini Saudi Arabia muongo mmoja uliopita.
Wanne akiwemo Nimr ni wa madhehebu ya Shia wanotuhumiwa kuwauwa polisi kwa kuwapiga risasi.
Hukumu hizo zimetekelezwa katika miji 12 nchini Saudi Arabia nne zimetekelezwa na magereza kwa kuwafyatulia risasi na nyengine kwa kukata vichwa.Hapo mwezi wa Disemba Al Qaeda katika Ghuba ya Arabuni ilitishia kulipiza kisasi dhidi ya Saudi Arabia kwa mauaji yoyote ya wanachama wake.
Iran na washirika wake wailani Saudia
Maadamano ya kupinga kutekelezwa adhabu ya kifo kwa Sheikh Nimr al-Nimr nchini Bahrain. (02.01.2016)
Maadamano ya kupinga kutekelezwa adhabu ya kifo kwa Sheikh Nimr al-Nimr nchini Bahrain. (02.01.2016)
Hasimu mkuu wa Saudi Arabia katika kanda hiyo Iran imelaani vikali kuuliwa kwa Nimr na kusema kwamba nchi hiyo italipa gharama kubwa.Polisi ya Saudi Arabia imeimarisha usalama katika kitongoji chenye Washia wengi.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Jaber Ansari amesema badala ya kuwalenga magaidi wa Dola la Kiislamu wanaotishia kanda hiyo na dunia nzima Wasaudi wamemuuwa kiongozi mashuhuri kama vile al-Nimr.Ansari ameliambia shirika la bahari la Iran ISNA kwamba kifo cha al-Nimr kimechochewa kisiasa na kidini.
Viongozi wa Kishia nchini Lebanon na Iraq pia wamelaani kuuliwa kwa al-Nimr.Wafuasi wanaomuunga mkono Nimr nchini Bahrain nchi inayotawaliwa na Wasunni lakini Washia ndio walio wengi,maadamano ya ghadhabu yamefanyika huku watu wakizilaani serikali zote mbili ya Saudi Arabia na Bahrain. Baadhi ya wandamanaji walipambana na polisi licha ya kuwa hakukuwa na maafa.
Taarifa ya serikali ya Saudi Arabia imesema watuhumiwa hao walipatikana na hatia ya kufanya mashambulizi tafauti dhidi ya vituo vya usalama na raia pamoja na kuwauwa maafisa wa usalama na raia nchini Saudi Arabia.
Adabu za kifo zilikuwa za haki
)Tangazo la televisheni Saudi Arabia juu ya kutekelezwa kwa adhabu ya kifo kwa Sheik Nimr all Nimr na watu wengine 46. (02.01.2016)
Tangazo la televisheni Saudi Arabia juu ya kutekelezwa kwa adhabu ya kifo kwa Sheik Nimr all Nimr na watu wengine 46. (02.01.2016)
Utetekelezaji huo wa adhabu ya kifo umekuja baada ya kuthibitishwa na mahakma kuu nchini humo na kuridhiwa na Mfalme Salman.Afisa wa ngazi ya juu wa sheria ya Kiislamu nchini Saudi Arabia Mufti Mkuu Abdel-Aziz al-Sheikh ameiambia televisheni ya taifa kuwa kutekelezwa kwa hukumu hizo kumefanyika kwa haki na kunakusudia kuimarisha usalama.
Hii ni mara ya kwanza mwaka huu kutekelezwa kwa adhabu ya kifo nchini Saudi Arabia ambayo inaaminika kuwa imetekeleza adhabu za kifo 137 mwaka jana kwa makosa mbali mbali.
Kutekelezwa sambamba kwa adahabu za kifo 47 kwa Wasaudi 45,raia mmoja wa Misri na mmoja wa Chad ni utekelezaji mkubwa kabisa wa hukumu hizo kwa makosa ya usalama kuwahi kushuhudiwa nchini humo tokea kuuliwa kwa waasi wa jihadi 63 hapo mwaka 1980 ambao waliuteka Msikiti Mtakatifu wa Mecca hapo mwaka 1979.
Harakati za Nimr
Maadamano ya kupinga kutekelezwa adhabu ya kifo kwa Sheikh Nimr al-Nimr nchini Pakistan.. (02.01.2016)
Maadamano ya kupinga kutekelezwa adhabu ya kifo kwa Sheikh Nimr al-Nimr nchini Pakistan.. (02.01.2016)
Al-Nimr mwenye umri wa miaka 55 mara kwa mara amekuwa akidai kuongezwa kwa haki za Washia walio wachache nchini humo ambao idadi yao ni kama asilimia 15 ya wananchi wa Saudi Arabia.
Alikuwa akikamatwa mara kwa mara kwa harakati zake za kupinga serikali.Kukamatwa kwake mara ya mwisho hapo mwaka 2012 kulichochea maandamano ya ghasia katika mji alikozaliwa wa Qatif ambapo kuna Washia wengi mashariki mwa Saudi Arabia.
Washia wa Saudi Arabia wanalakamika kwa kubaguliwa na wanasema mara nyingi wamekuwa imekuwa vigumu kupata nyadhifa za juu serikalini na mafao mengine wanayopata raia wengine.
Kusudio la hukumu
Utekelezahi wa adhabu hizo za kifo unakusudia zaidi kutowashajiisha Wasaudi na harakati za kijihadi kufuatia miripuko ya mabomu na mashambulizi ya risasi yaliofanywa na wanamgambo wa itikadi kali nchini Saudi Arabia mwaka jana na kuuwa watu kadhaa wakati huku kundi la Dola la Kiislamu likitowa wito kwa wafuasi wake kufanya mashambulizi nchini humo.
Familia ya utawala wa kifalme ya Al Saud imezidi kuwa na wasi wasi katika miaka ya hivi karibuni kutokana na machafuko yalizogaa Mashariki ya Kati hususan nchini Syria na Iraq ambapo wapiganaji wa jihadi wa Kisuni wamepata nguvu na kutowa fursa kwa Iran nchi ya Kishia kueneza ushawishi wake.
Taarifa ya serikali iliotangaza kutekelezwa kwa adhabu hizo za kifo ilianza kwa aya za Quran zenye kuhalalisha matumizi ya adhabu ya kifo na televisheni ya taifa ikaonyesha hali ilivyokuwa baada ya mashambulizi ya Al Qaeda muongo mmoja uliopita.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni