Watu 27 wamefariki dunia katika shambulio la hoteli ya kitalii ya Splendid katika mji mkuu wa Burkina Faso , Ouagadougou.
Taarifa
zaidi zinasema kuwa watu wengine 126 wamefanikiwa kuokolewa na vikosi
vya kijeshi vya nchi hiyo vikisaidiwa na wanajeshi wa Ufaransa baada ya
kuizingira hoteli hiyo kwa muda baada ya kuvamiwa na kutekwa na
wapiganaji wanne waliokuwa na silaha nzito.
Kundi la Al-Qaeda la islamic Maghreb{AQIM} limedai kuhusika katika tukio hilo.
Hoteli
hiyo ilitekwa kwa muda wa saa 15 kabla ya vikosi vya kijeshi kuingilia
kati na kufanikiwa kuwaokoa watu hao. Watu 23 wa mataifa 18 tofauti
walifariki katika tukio hilo.
Wanajeshi wakiwa tayari kwa lolote walipoizingira hoteli hiyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni