Chelsea imepata ushindi wake wa kwanza ikiwa chini ya Kocha Guus Hiddink baada ya kuitungua Crystal Palace kwa mabao 3-0 na kukwea juu kulikimbia kundi la kushuka daraja.
Oscar aliipa Chelsea bao la kwanza na baada ya kufunga bao hilo Chelsea ilitawala mchezo na kuongeza bao la pili kupitia kwa Willian.
Costa alikamilisha ushindi huo katika dakika ya 66 baada ya wachezaji wa Crystal Palace kushindwa kuokoa shuti la Willian. Katika mchezo mwingine Everton 1-1 Tottenham.
Willian akipachika bao la pili kwa Chelsea
Diego Costa akipachika bao tatu kwa Chelsea
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni