MTAA WA GONGO LA MBOTO MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM WAENDELEA KUUNGA MKONO KAULI YA RAIS DK.MAGUFULI YA KUFANYA USAFI

 Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na kufanya usafi katika Mtaa wa Gongo la Mboto Manispaa ya Ilala,  Ali Mwinyimkuu (kulia), akishiriki kufanya usafi na wananchi Dar es Salaam jana, ikiwa ni utaratibu waliojiwekea wa kufanya usafi kila baada ya wiki mbili ili kuunga mkono kauli Rais Dk. John Magufuli ya kufanya usafi katika maeneo tunayoishi na kufanyia shughuli zetu nchini.
 Kazi ya usafi ikiendelea.
 Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na kufanya usafi katika Mtaa wa Gongo la Mboto Manispaa ya Ilala,  Ali Mwinyimkuu Omari akiwaongoza wenzake kufanya usafi.
 Hapa ni kazi tu tunaukataa uchafu.
 Wanawake wakishiriki kufanya usafi eneo la relini.
 Mwenyekiti wa Mtaa huo, Bakari Shingo (Aliyevaa kaputura), akishiriki kufanya usafi na wananchi wake Dar es Salaam jana, ikiwa ni utaratibu waliojiwekea wa kufanya usafi kila baada ya wiki mbili ili kuunga mkono kauli Rais Dk. John Magufuli ya kufanya usafi katika maeneo tunayoishi na kufanyia shughuli zetu nchini.
 Usafi ukiendelea.
Wasanii wa Kikundi cha Rock Star wa Mtaa huo nao walishiriki kufanya usafi.

Na Dotto Mwaibale

WANANCHI wa Mtaa wa Gongolamboto Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameendelea kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa kufanya usafi katika eneo hilo kwa wiki mara mbili ili kuyaweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea mtaa huo Dar es Salaam jana kujionea shughuli za usafi katika eneo Mwenyekiti wa mtaa huo Bakari Shingo alisema lengo lao kubwa ni kuiunga mkono kauli ya Rais Magufuli ya kufanya usafi ambapo wao wameamua kufanya usafi kwa wiki mara mbili.
Alisema lakini wao walianza kufanya usafi katika eneo kabla ya rais kuanza kuhimiza lakini kauli ya Magufuli ilichochea zaidi moto wa kufanya usafi kwa wananchi wa eneo hilo.
Shingo alisema katika mtaa wao kunavikundi ambavyo vinasaidia kufanya usafi ambapo wamegawa maeneo  na utaratibu huo umesaidia kuyaweka mazingira katika hali ya usafi.
Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na usafi katika mtaa huo Ali Mwinyimkuu  Omari alisema kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa katika suala zima la usafi katika eneo hilo kutokana na utaratibu waliojiwekea.
Alisema wanamshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Issaya Mngulumi kwa kujitoa kwake kuwapa gari la kusomba takataka kila wanapofanya usafi hali ambayo inawapa moyo wananchi wa kufanya usafi hivyo kumungana mkono Rais Dk. John Magufuli katika suala zima la usafi nchini.

JOVAGO TZ YAWATAKA WATANZANIA KUTUMIA INSTAGRAM KUTANGAZA UTALII.

Meneja wa mawasiliano wa Jovago,Liliani Kisasa akizungumza na waandishi wa habari juu ya kutumia mitandao ya kijamii kwa maendleo ya Taifa katika mkutano uliofanyika kinondoni jijini Dar es Salaam.


TAASISI ya kufanya Biashara mitandaoni ya Jovago Tanzania imewataka watanzania kutumia fursa ya matumizi ya mitandao ya kijamii kuitangaza nchi katika sekta ya utalii kimataifa.

Wito huo imetolewa na Mkurugenzi wa Jovago Afrika Mashariki Estelle Verdier –Watine alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya umuhimu wa matumizi ya mtandao wa Instagram kutangaza utalii wa Tanzania.

“Tanzania ni nchi inayoongoza kwa matumizi ya instagram Africa hivyo fursa hiyo ni vyema ikatumika vyema katika kupandisha utalii wa taifa hili kuliko kupost vitu ambavyo avina faida kwa taifa” alisema Estelle.

Alisema kuwa kwa kuthamini hilo tasisi ya Jovago Tanzania imeandaa shindano la kuweka pichakatika Insrgram hivyo atakaye pata like nyingi ataweza kupata ofa ya kulala katika Hotel ya Ramada iliyopo Mbezi Beacha Dar es Salaam.
Kwa upande wake afisa habari wa kampuni hiyo Liliani Kisasa aliwatka watanzania kuchangamkia fursa hiyo hili waweze kufurahia siku hiyo wakiw ana wenzi wao.

Alisema ni jambo zuri sana kama mmoja ya watu kutoka hapa nchini.
Liliani Kisasa PR manager Jovago.
Liliani Kisasa PR manager Jovago.
Estelle Verdier -Watine East Africa Manger Jovago .Com akizungumza na wana habari.
Liliani Kisasa PR manager Jovago akiojiwa na ITV.

Wanakijiji Mungere kupewa bure miche ya miti kukabili maafa ya upepo

Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki akimuongoza Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya kukagua athari za upepo kwa mashamba ya migomba kijiji cha Mungere, wilayani Monduli, tarehe 31 Januari , 2016.
Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki akionesha sehemu ya mgomba iliyoanguka baada ya upepo mkali kuathiri shamba lake la ekari 3, wakati Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, ilipokuwa ikikagua athari za maafa hayo katika kijiji cha Mungere, wilayani Monduli, tarehe 31 Januari , 2016.
akimueleza jambo Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki mara baada ya kukagua athari za upepo kwa mashamba ya migomba katika kijiji cha Mungere, wilayani Monduli, tarehe 31 Januari , 2016.
Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki akimuonesha Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya baadhi ya ndizi zilizo katwa kwenye migomba iliyoanguka baada ya upepo mkali kuathiri shamba lake la ekari 3, wakati Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, ilipokuwa ikikagua athari za maafa hayo katika kijiji cha Mungere, wilayani Monduli, tarehe 31 Januari , 2016.
Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki akimshika bega Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya kama ishara ya kumshukuru mara baada ya kukagua athari za maafa ya upepo mkali katika kijiji cha Mungere, wilayani Monduli, tarehe 31 Januari , 2016.
Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki akimuonesha Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya maeneo upepo mkali ulioleta maafa katika mashamba ya migomba katika kijiji cha Mungere, wilayani Monduli, mara baada ya kukagua athari za maafa hayo , tarehe 31 Januari , 2016. (Picha na Ofisi ya Wazairi Mkuu )

Na. Mwandishi maalum

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa itatoa mbegu bure za miti ili kukabili maafa ya upepo mkali kwa wakazi 3,000 wa kijiji cha Mungere, ambao mashamba yao ya migomba yalikumbwa na maafa ya upepo mkali uliosababisha ekari 250 kati ya ekari 300 za mashamba hayo kuathiriwa  na upepo huo.

Akiongea wakati wa ziara ya kukagua athari za maafa hayo katika kijiji cha Mungere, wilayani Monduli Tarehe 31 Januari, 2016, Mkurugenzi wa Idara ya uratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya amebainisha kuwa serikali imeamua kuwagawia bure mbegu za miti itakayopandwa kwa kuzunguka mashamba yao ili waweze kukabili maafa hayo ya asili.

“Ofisi ya Waziri Mkuu idara ya uratibu maafa inalojukumu la kuratibu shughuli za maafa katika hali ya kujiandaa, kuzuia, kukabili na kurudisha hali ya kawaida pindi maafa yanapotokea kwa hapa kijijini Mungere tumeamua kukabili maafa yatokanayo na upepo kwa kuwapa wakulima wa zao la ndizi waweze kuipanda miti hiyo itakayowezesha kupunguza kasi ya upepo mkali ambao husababisha migomba kuanguka katika mashamba yao.” amesema Brig. Jen. Msuya

Msuya aliongeza kuwa  idara yake  itatoa chakula cha msaada kwa waathirika wa maafa hayo ili waweze kuwa na chakula cha kutumia wakati  baadhi ya migomba yao iliyoathirika ikiendelea kuchipuka  na mingine kukomaa ambapo wataweza kupata chakula lakini pia  na kujipatia fedha kwa kuuza zao hilo.
Awali akiongea katika ziara hiyo, Alaigwanani wa mila, Saibulu Olemariki alifafanua kuwa upandaji miti ndio njia pekee ya kuwajengea uwezo wakulima wa zao la ndizi kuweza kukabili maafa ya upepo katika kijiji hicho kwa kuwa mashamba yao yamekuwa yakikumbwa na maafa ya upepo mkali ambao umekuwa ukiangusha migomba ambayo tayari inakuwa imeshabeba ndizi kubwa na zilizo komaa.

“Kama kiongozi wa kimila nitawahamasisha wanakijiji wenzangu hasa wakulima wa mashamba ya migomba kuhakikisha kuwa kila mtu anazungusha miti ya kutosha katika shamba lake lakini pia kuhakikisha kuwa miti hiyo inatunzwa kwa kuimwagilia maji na kutokatwa ovyo.” alisisitiza Alaigwanani Olemariki.

Alaigwanani Olemariki alieleza masuala yanayo kuwa kikwazo kwa wakulima hao kuwa ni  miundo mbinu ya barabara na Umwagiliaji kwa kueleza  kuwa pamoja na kijiji hicho kuwa na maafa ya upepo ambayo huathiri mashamba yao ya migomba lakini pia miundo mbinu ya barabara imekuwa kikwazo cha wakulima hao kwa kushindwa kusafirisha ndizi ili waweze kulifikia soko kwa wakati .

“Tunaomba serikali iweze kuiboresha barabara inayokuja kijijini hapa ili kuweza kuhamasisha wafanyabiashara wengi kufika kijijini hapa kununua ndizi kwa kuwa kama tunakuwa hatujapatwa na maafa tunaouwezo wa kuzalisha ndizi nying na hili niombe serikali kuwa sisi tunazalisha ndizi nyingi amabazo tukijengewa mazingira mazuri ya kilimo chetu ikiwa ni pamoja na kujengewa mfereji bora wa maji tunao uwezo wa kuilisha Monduli nzima na hata nje ya hapo.” alisisitiza Alaigwanani Olemariki.

BALOZI SIMBA AWAPONGEZA WAOKOAJI AJALI YA MV KILOMBERO, AMALIZA ZIARA YAKE YA KUTEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO YA JESHI LA MAGEREZA MKOANI MOROGORO.

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati) pamoja na ujumbe wake, wakiingia katika lango kuu la kuingilia abiria wakati alipotembelea eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero II na kushuhudia shughuli za uokoaji wa magari, utafutaji miili ya watu na uokoaji wa kivuko hicho ukiendelea. Balozi Simba alifanya ziara ya kikazi mkoani Morogoro kwa kutembelea miradi ya maendeleo ya Jeshi la Magereza mkoani humo.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia), akisalimiana na Askari wa Kikosi cha Wanamaji wa Uokoaji wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambao wanashiriki katika shughuli za uokoaji miili ya watu waliozama baada ya kivuko cha MV Kilombero II kuzama Januari 27.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akiongozana na ujumbe wake kuelekea eneo la tukio ambapo kivuko cha MV Kilombero II kilizama wiki iliyopita. Kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa. Katikati ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, SACP Dkt. Kato Lugainunura.
 Katibu Tawala Wilaya ya Kilombero, Yahya Naniya (kulia), akitoa maelezo juu ya shughuli za uokoaji zinavyoendelea kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (wa tatu kushoto) na ujumbe aliofuatana nao mara baada ya kufika eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero II wiki iliyopita. Naibu Katibu Mkuu alikuwa mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki kwa ziara ya kikazi.
 Wasamaria wema waliojitolea kushiriki zoezi la uokoaji katika ajali ya kivuko cha MV Kilombero II kilichotokea wiki iliyopita mkoani Morogoro, wakimuelekeza dereva wa gari la kunyanyua vitu vizito (halipo pichani), wakati wa uokoaji wa moja ya magari yaliyozama wakati wa ajali hiyo.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto) na ujumbe aliofuatana nao wakiangalia shughuli za uokoaji zinavyoendelea mara baada ya kivuko cha MV Kilombero kuzama huku baadhi ya vitu vikiokolewa.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, akiondoka eneo kilipozama kivuko cha MV Kilombero mara baada ya kushuhudia shughuli za uokoaji zikiendelea vizuri.

BENKI YA CRDB YATOA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU YA BUNGE.

NA MWANDISHI WETU, DODOMA
BENKI ya CRDB imetoa msaada wa vifaa vya michezo kwa wabunge wa Jamhuri la Muungano wa Tanzania.

Vifaa hivyo vilikabidhiwa na Mkurugenzi wa benki ya CRDB Tawi la Dodoma, Rehema Hamis na kupokelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni jezi seti mbili ikiwamo ya golikipa, viatu, mpira, soksi na suti za michezo ambavyo vimegharimu zaidi ya Sh. Milioni 5.
Awali Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliwapongeza wafadhili na wadhamini wanaojitokeza kusaidia sekta ya michezo na kuwataka wengine waige mfano huo, kwani hivi sasa michezo ni uchumi.
Kwa upande wake Mkurugenzi kutoka makao makuu ya CRDB anayeshughulikia Mikakati na Ubunifu, Goodluck Nkini, alisema wameamua kutoa vifaa hivyo kutokana na mapenzi yao kwa wananchi hususan wateja wao, ambao wabunge ndio wawakilishi wao.
“Pia ni katika mpango wa taasisi kuunga mkono katika kazi, kwani michezo mbali ya burudani hujenga afya, hivyo wabunge na wafanyakazi wa CRDB wakiwa na afya njema watatekeleza vema majukumu yao,” alisema Nkini. 
Jioni ulipigwa mchezo wa kirafiki kati ya Bunge FC na CRDB kwenye Uwanja wa Jamhuri na kumalizika sare ya bao 1-1.
Walikuwa ni CRDB walioanza kuzifumania nyavu za Bunge FC dakika ya 49 mfungaji akiwa Faisal Mbuya.
Bunge FC walicharuka na kuwachukua dakika sita tu kuchomoa dakika ya 55 kwa bao la Yusuf Gogo. Hadi mwamuzi Peter Mdachi akipuliza kipenga kuashiria dakika 90 kumalizika, hakuna aliyeibuka mbabe. 
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa vya michezo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akipokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis kwa ajili ya timu ya soka ya Bunge. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni Naibu Spika Dk. Tulia Akson, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa na kushoto ni Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Goodluck Nkini. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea viatu vya michezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akipokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis kwa ajili ya timu ya soka ya Bunge. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni Naibu Spika Dk. Tulia Akson, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa na kushoto ni Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Goodluck Nkini. 
Waziri Mkuu akipokea mpira.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Mkurugenzi wa Mikakati na Ubunifu wa Benki ya CRDB, Goodluck Nkini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Meneja wa Biashara wa Benki ya CRDB, Daniel Shemdoe. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa Benki ya CRDB pamoja na maofisa wa benki hiyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma, Rehema Hamis akimsiliza kwa makini Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa benki, hiyo, Willy Kamwela.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi yao na Wabunge.
Wachezaji wa CRDB wakiwa katika mazoezi kabla ya mchezo wao.
Baadhi ya wachezaji wa Benki ya CRDB wakitoka uwanjani.
Wachezaji wa Bunge FC wakiwa katika mazoezi.
Naibu Spika Dk. Tulia Akson akikagua timu ya Benki ya CRDB.
Naibu Spika Dk. Tulia Akson akikagua timu ya Bunge.
Wachezaji wa timu ya Bunge wakisalimiana na wachezaji wa Benki ya CRDB.
Kikosi cha timu ya Bunge.
Kikosi cha timu ya Benki ya CRDB.
Nahodha wa timu ya Bunge, William Ngeleja (kushoto), akichuana na mchezaji wa Benki ya CRDB, Chande Ismail katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Nahodha wa timu ya Bunge, William Ngeleja akimiliki mpira. Kulia ni Chande Ismail.
Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto akimiliki mpira.

TANZANIA KUWACHUKULIA HATUA ZA KINIDHAMU NA KISHERIA MAHAKIMU 508 WALIOTEKELEZA MAJUKUMU YAO CHINI YA KIWANGO. ASEMA JAJI MKUU MHE. MOHAMED CHANDE OTHMAN



 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed  Chande Othman akizungumza wa waandishi wa Habari kuhusu kuanza kwa Mwaka wa Sheria 2016, Wiki ya Sheria na Utendaji wa Mahakama ya Tanzania kwa mwaka 2016. Wengine Kushoto ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu (Kushoto) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaaban Lila (kulia).
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kushoto) akiwa ameambatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu (Katikati) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaaban Lila (kulia) wakielekea kwenye mabanda ya Maonesho ya Wiki ya Sheria  kwa mwaka 2016  katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo kilele cha Wiki hiyo kitakuwa Februari 4 2016 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
 Baadhi ya Wananchi wakipata huduma katika mabanda ya maonesho wakato wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akitembelea banda la maonesho la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini leo viwanja vya Mnazi mmoja.

Na Aron Msigwa –  MAELEZO
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman amesema kuwa Mahakama ya Tanzania itawachukulia hatua za kinidhamu na za kisheria Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo,Wilaya na wale wa Mahakama za Hakimu Mkazi wapato 508 kote nchini waliotekeleza majukumu yao chini ya kiwango na kushindwa kutimiza wajibu wa Mahakama wa Utoaji wa Huduma Bora kwa wananchi katika mwaka wa Sheria wa 2015/2016.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam alipokua akitoa ufafanuzi kuhusu  kuanza kwa mwaka mpya wa Sheria wa 2016 na Maadhimisho ya Wiki ya Sheria ambayo kilele chake kitakua Januari 4,2016 Mhe.Othman amesema  kuwa kwa mujibu wa taratibu za uendeshaji wa Mahakama na upimaji wa viwango vya utendaji kazi vilivyowekwa, Mahakimu hao wa Mahakama za wilaya na Hakimu Mkazi 121 na 387 wa Mahakama za Mwanzo watatakiwa  kutoa maelezo ndani ya siku 7 juu ya sababu zilizowafanya washindwe kutimiza lengo lililowekwa la kushughulikia mashauri 260 kila mmoja.
Amesema watakaothibitika  kamati za nidhamu na maadili za kila wilaya na Mikoa ambazo ni Kamati ndogo za Tume ya Utumishi wa Mahakama zitawafungulia kesi za kinidhamu ndani ya siku 21.
“Wale watakaobainika watakumbwa na adhabu ya kupewa Onyo, kushushwa vyeo na kufukuzwa kazi ili iwe fundisho kwa wengine, ninajua wapo baadhi ambao waliajiliwa katikati ya mwaka, wengine kwenda mafunzo ya vitendo vyuoni, wajawazito na baadhi vituo vyao kuwa na kesi chini ya 260 kwa mwaka” Amesisitiza.
Aidha, katika hatua hiyo amewapongeza Mahakimu waliofanya vizuri katika utendaji wao wakiwemo 14 walioshughulikia mashauri zaidi ya 700 kila mmoja, Mahakimu 50 walioamua kesi zaidi ya 500 kila mmoja baadhi wakitokea wilaya ya Mkuranga, Rufiji  na Bukoba mjini na wengine wawili kutoka Dar es salaam walioamua kesi zaidi ya 900 kila mmoja na  kuvuka lengo la utendaji lililowekwa la kushughulikia mashauri 260 kwa mwaka.

Akitoa tathmini ya utendaji wa Mahakama kwa mwaka wa sheria uliopita amesema kuwa Mahakama ya Tanzania ina Mahakama za Hakimu Mkazi kila Mkoa na Mahakama za Wilaya 111 katika wilaya za Kiserikali 133 pamoja na Mahakama za Mwanzo ambazo hupokea asilimia 93 ya mashauri yanayofunguliwa kote nchini.
 Amesema mwaka 2015 Mahakama zote nchini zilipokea jumla ya mashauri 206,115, kati ya hayo mashauri 220,815 yaliamuliwa kukiwa na ziada ya mashauri 14700 jambo linaloonyesha kuwa Mahakama zinapokea mashauri na kuyashughulikia kwa kasi inayoridhisha huku mashauri yanayosababisha mrundikano ni yale yaliyo nje ya idadi iliyopangwa.

Ameongeza kuwa katika katika kipindi cha mwaka huo wa 2015 Mahakama za Mwanzo zilipokea mashauri 141,025 ambapo kati ya hayo Mashauri 149,757 yalishughulikiwa huku idadi ya Mahakimu walioshughulikia mashauri hayo ni 1240.
“Ukiangalia mwenendo wa ufunguaji wa mashauri yote kote nchini hasa Tanzania Bara utagundua kuwa Mahakama za Mwanzo, Wilaya na zile za Hakimu Mkazi  zinapokea mashauri mengi kwa asilimia 93 ,katika kila mashauri 4 yanayofunguliwa nchini 3 yako mahakama za mwanzo ambako wananchi wengi wanatafuta ufumbuzi wa kesi zao lazima tuweke mkazo” Amesema Jaji Mkuu Mhe.Othman.
Kuhusu kuanza kwa mwaka mpya wa Sheria mwaka 2016 amesema Mahakama inauanza chini ya Kauli Mbiu Isemayo “Huduma Bora kwa Wananchi ni Wajibu wa Mahakama na Wadau wake”  ikiwa na kesi 20,431 ikilinganishwa na 34,126 ilizoanza nazo mwaka 2015 na kuongeza kuwa licha ya changamoto zinazoikabili Mahakama ya Tanzania mkakati uliopo ni kupunguza idadi hiyo hadi kufikia 0 kwa kila mwanzo wa mwaka wa sheria.

Akitoa ufafanuzi kuhusu upatikanaji wa Nakala za hukumu amesema Serikali inaendelea kuijengea uwezo wa kifedha Mahakama wa kuajiri wachapaji wa nakala wengi zaidi ili Nakala za Hukumu za Kesi ziweze kupatikana pindi tu kesi zinapomalizika katika mahakama zote nchini tofauti na ilivyo sasa ambapo hupatikana Mahakama Kuu na Mahakama za Rufani

Aidha, amesema Mahakama inaendelea kuboresha miundombinu yake ikiwemo majengo na ujenzi wa mahakama mpya katika maeneo yasiyo na huduma hiyo katika mwaka 2016. “ Hivi sasa tuna wilaya 23 hazina Majengo ya Mahakama za wilaya, kwenye baadhi ya maeneo kesi zinasikiliziwa Ofisini kwa Hakimu wakati ilitakiwa ziwe kwenye jengo lenye ukumbi wa wazi,tumejiandaa kwa michoro ya majengo kwa mahakama zote ili tuanze kujenga kwa gharama nafuu”  
Mhe. Othman ametoa wito kwa wananchi kutosita kuitumia Mahakama ya Tanzania katika kupata ushauri wa kisheria kupitia wataalamu wake, kuhudhuria maonesho mbalimbali ya kisheria yanayofanyika nchini huku akitoa angalizo kwa baadhi ya watu wanaochangia kuwepo kwa mrundikano wa kesi kwa kufungua kesi za madai au kupeleka mashauri Mahakamani kama sehemu ya maegesho ya masuala yao.

“Baadhi ya watu wamekuwa wakipeleka kesi Mahakamani kama sehemu ya maegesho, huzifungua kisha hushindwa kujitokeza Mahakamani hizi ni tofauti na zile zenye vipengele vingi ndani ya kesi moja au zile ambazo mashahidi wake wamehama kutoka eneo moja kwenda linguine, hizi nawahakikishia tutazifuta ili kupunguza mrundikano wa kesi kwenye Mahakama zetu” Amesisitiza Mhe. Othman.

TAASISI YA MANJANO FOUNDATION YAWAKOMBOA WANAWAKE WA ZANZIBAR KIUCHUMI

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation mama Shekha Nasser .
Taaasisi ya Manjano Foundation inaendesha mafunzo ya siku 5 kwa Wanawake wa mjini Zanzibar. Taasisi hiyo inaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa lengo la kumkomboa mwanamke aweze kujiongezea kipato na kukua kiuchumi.Katika mafunzo hayo yanayoendelea kwenye Hotel ya Mtoni Marine Zanzibar wanawake  hao watapatiwa elimu namna ya kuanzisha na kuendesha biashara. Pia watajifunza  namna ya kujiwekea akiba na kutafuta masoko na kutoa huduma bora kwa wateja wao. 
Mwisho wa mafunzo haya washiriki wote watakopeshwa mitaji kwa ajili ya kuanzisha na  kuendesha biashara zao. Katika hatua nyingine washiriki wa mafunzo hayo waliojitokeza kwa wingi wameishukuru Taasisi ya Manjano Foundation kwa kuwakomboa na mafunzo ya kiuchumi na kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira.
Washiri wa mafunzo hayo..
Mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu mbili, katika awamu ya kwanza  washiriki watapewa mbinu mbalimbali za kuanzisha na kuendesha biashara, pia kuwapa uwezo wa kutambua nafasi yao kwenye jamii wakiwa kama wanawake na kuondoa woga wa kujihusisha na kufanya kazi kwa juhudi na weledi katika biashara zao ambapo Mkufunzi wa masomo hayo ya maswala ya Biashara ni Mama Salma Salim Omar wa Zanzibar Chamber of Commarce.
  
Baadaye mtaalamu wa maswala ya urembo na matumizi ya sahihi ya vipodozi Mama Shekha Nasser atatoa ujuzi wa matumizi ya vipodozi pendwa vya LuvTouch Manjano, mfano kupamba maharusi na utunzaji wa ngozi.
Picha ya Pamoja ya Wanawake wa Zanzibar 
waliojitokeza kwenye Mafunzo ya Ujasiriamali.